HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 9 September 2017

Arusha,Dodoma na Tunduma wafurahia miaka 40 ya Safari Lager

Mchoma nyama wa akiachoma Kuku wakati wa shamra shamra za maadhimisho ya miaka 40 ya Safari Lager yaliyofanyika Cape Town Complex mwishoni mwa wiki.
Wakazi wa Dodoma wakifura na bia ya Safari Lager wakati wa maadhimisho ya miaka 40 ya Safari Lager yaliyofanyika Cape Town Complex mwishoni mwa wiki. 

WAKAZI wa Arusha, Dodoma na Tunduma wafurahia shamra shamra miaka 40 ya Safari lager kwa nyaka tofauti tofauti mwishoni mwa wiki.

Baada ya uzinduzi rasmi wa maadhimisho ya miaka 40 ya Safari Lager tangu kuanza kuzalishwa kwake hapa nchini mwaka 1977 sasa shamra shamra hizo zimehamia mikoani  ambapo mwishoni mwa wiki hii wakazi wa Arusha walijumuika katika Bar ya Picnic ambapo ilikuwa funga mtaa mitaa ya Kaloleni.

Wakati huo huo, wakazi wa Dodoma walijumuika katika maadhimisho hayo maeneo ya Cape town Complex na kule Tunduma shamra shamra hizo zilitanda  maeneo ya Olimpia.

Akizungumzia sherehe hizo Meneja wa bia ya Safari Lager Bi. Edith Bebwa  alisema kuwa hatua ya mafanikio iliyofikiwa na bia ya Safari ni ya kujivunia na hasa kwa sababu bado inaendelea kuwa moja ya kinywaji kinachopendwa zaidi katika soko lenye vinywaji vingi vya aina ya bia.

“Safari Lager ni bia inayoongoza kwa tuzo za ubora wa kimataifa na inaendelea kuwa bia inayopendwa nchini kwasababu ya ubora wa hali ya juu na zaidi hasa kwa sababu ya wateja wetu. Tumeandaa burudani ili kuwashukuru wateja wetu kwa sapoti yao kwa bia yetu hii halisi ya kitanzania.”

Bia ya Safari Lager ni bia yenye miaka mingi katika soko la Tanzania yenye tuzo nyingi za dhahabu ( Gold Monde Selection) na mwaka 2014 Safari lager ilipata tuzo ya hali ya juu ya Monde Selection kwa kuwa bia bia yenye tuzo nyingi za dhahabu za Monde Selection.

 “Tunajivunia kuwa nchini kwa miaka 40 na bado bia ya Safari Lager ikiwa ni chaguo namba moja la Watanzania. Tunawaalika wateja wetu wote na wapenzi wa Safari Lager waje kusheherekea nasi tutakapokuwa tukija mikoani kama hivi". aliongezea Edith.

Safari Lager ina mtazamo wa tofauti kwani huzingatia ilikotoka na misingi inayoifanya kuwa imara na kuendelea kusonga mbele na ndiyo maana inasherehekea miaka 40 huku ikitazama mbele kwa kusema #40NABAADO

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad