HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Sunday, 10 September 2017

TANZIA: KAMISHNA MSTAAFU WA OPERESHENI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI KUAGWA LEO JIJINI DAR ES SALAAM.


Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini – Thobias Andengenye, ataongoza Maafisa na Askari katika zoezi la kuuaga mwili wa Marehemu na kutoa heshima za mwisho (Kwa Paredi Maalum), kwa aliyekuwa Kamishna Mstaafu wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji CF (OPS) Rogatius Peter Kipali, ambaye alifariki dunia Semptemba 7, 2017 akiwa nyumbani kwake Mombasa, Ukonga Jijini Dar es Salaam.

Zoezi la kuuaga mwili wa Marehemu litafanyika leo Semptemba 10, 2017 kuanzia saa 3:00 asubuhi katika viwanja vya Kituo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Ilala eneo la FIRE barabara ya Morogoro Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji anapenda kuvitaarifu Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Maafisa, Askari na Watumishi wote wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, , familia ya Marehemu na wale wote walioguswa na msiba huu kwa namna moja au nyingine kujitokeza kwa ajili ya kutoa heshima zao za mwisho.

IFUATAYO NI RATIBA NZIMA YA MSIBA
Bwana alitoa na bwana ametwaa, jina la bwana lihimidiwe
Amina.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA-JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad