HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Sunday, 17 September 2017

Anna Marrica azindua mradi wa sauti ya vijana MYIDC Temeke

Afisa maendeleo ya vijana Temeke, Anna Marrica   akizungumza na vijana wa mradi wa  sauti ya  vijana  MYIDC na kuwapongeza kwa hatua waliofikia na kuwataka wasikate tamaa katika swala la kutafuta  maendeleo. Uzinduzi huo ulifanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Temeke jijini Dar es Salaam .
Mwenyekiti Mtendaji MYIDC,  Ismae  Mnikite akizungumza na vijana wa mradi wa MYID  pamoja na kudadafua zaidi lengo la uzinduzi huo ni  nikulenga  kuanzisha na  kuendeleza  majukwaa  ya vijana  kuanzia ngazi ya  kata nne 4 ambazo ni Buza, Mkangarawe, Kilakala na Tandika, leo Jijini   Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi msaidizi  mafunzo  na maendeleo ya ujuzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Julius Tweneshe akizungumza na vijana wa mradi wa MYID kwa kutoa wito katika kuchangamkia fursa zinazojitokeza hapa nchini.
Afisa Habari wa chama cha mbio za polepole Manispaa ya Temeke (Jogging) akiuliza swali  kwa Mkurugenzi msaidizi mafunzo na maendeleo ya ujuzi kutoka ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Julius Tweneshe.
Vijana wa Mradi wa sauti ya vijana MYID wakisikiliza kwa makini mazungumzo ya viongozi wakati wauzinduzi wa mradi wa sauti ya vijana MYID uliofanyika katika harmashauri ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Picha ya  pamoja wakiwa ni viongozi, vijana wa mradi wa  sauti ya  vijana MYID, wageni waalikwa pamoja na waandishi wa habari.

Afisa maendeleo ya vijana Temeke, Anna Marrica  amezindua mradi wa  sauti ya  vijana katika Halmashauri ya wilaya ya Temeke na kuwataka vijana hao kutokata tamaa katika kutafuta maendeleo  ili kujikwamua  kiuchumi.
Marrica amesema hayo katika uzinduzi wa mradi uliofanyika  kwenye ukumbi wa manisapaa ya Temeke, lengo likiwa ni kutaka kuwapa moyo na kuwapongeza  vijana hao  kwa hatua nzuri  waliofikia  katika kuhakikisha wanaleta  maendeleo ambapo mradi huo umelenga  kuanzia ngazi ya kata ambazo ni Buza, Makangarawe, Kilakala pamoja na Tandika.
Nae Mwenyekiti Mtendaji MYIDC,  Ismae  Mnikite amesema kuwa lengo pia ni kutaka  kuishawishi  Halmashauri ya Manispaa  hiyo kufanya mchakato wa kutoa taratibu huru za wazi zinazofaa kuwaingiza vijana  katika mfumo rasmi  wa kutoa maamuzi  ikiwemo kushirikisha  hatua mbalimbali za uundwaji wa baraza la vijana  kunzisha nganzi ya kata  na hata hadi kiwilaya kwa mujibu wa tamko la sera ya Taifa ya maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007.
Vile vile  Mratibu wa mradi  MYIDC, Kissango Mario ametanabaisha kuwa upo umuhimu  wa vijana kujengewa uwezo wa  kuhamasishwa, utetezi na ushiriki katika maamuzi pamoja na kuandaliwa kimaadili
Hata hivyo Kaimu Mkurugenzi msaidizi mafunzo  na maendeleo ya ujuzi kutoka ofisi ya Waziri mkuu kazi vijana  ajira  na wenye ulemavu, Julius Tweneshe amesema kuwa Serikali inathamini  na kutambua mchango wa vijana hasa katika swala la kimaendeleo  na  ametoa ame toa wito kwa vijana wachangamkie fursa mbalimbali zianazojitikeza.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad