HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 16 September 2017

KAMA ULIPITWA NA MBIO HIZI ZA MBUZI NIMEKUWEKEA PICHA KIBAO HAPAMbuzi wakipigana vibega wakati wakitimua mbio kutafuta mshindi wa shindano lililopewa jina la 'The Southen Sun Fillies Frolic' lililodhaminiwa na Hoteli ya Southen Sun, wakati wa mashindano ya mbio hizo za mbuzi kwa mwaka 2017, yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Farasi, jijini Dar es Salaam leo na kihudhuliwa na wadau mbalimbali. Mashindano haya ya mbio za mbuzi huadhimishwa kila mwaka hapa nchini ikiwa ni sehemu ya kuchangisha fedha za kusaidia jamii mbalimbali zenye uhitaji.
Mbuzi wakiendelea kutimua vumbi katika mchuano mkali.
Safari ikielekea ukingoni.
Mmoja wa Mbuzi akiwa kabebwa baada ya kushindwa mbio hizo na kugoma kutembea.
Mbuzi Bingwa wa 'The Southen Sun Fillies Frolic' akipongezwa na wadau.
Shangwe tupu baada ya kuibuka kidedea.

Mwenyekiti wa kamati ya Mbio za Mbuzi, Bi. Karen Stanley akiwa pamoja na Viongozi wa Taasisi ya Doris Mollel.


Washiriki wa shindano la mavazi wakijinadi ili kujaribu bahati zao. Mbio za mwaka huu zilikuwa na kauli mbiu ya ‘Bollywood’ ambayo ni kiwanda cha filamu cha India, hivyo washiriki wengi walivaa mavazi yenye asili ya watu wa nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad