HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 23 August 2017

UBALOZI WA KUWAIT WAANZISHA MRADI “KITUO CHA KOMPYUTA KATIKA KILA TAASISI YA ELIMU”

 Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al-Najem kwakushirikiana na  Mkuu wa taasisi ya taaluma ya maendeleo Profesa  Esta  Dugumaro, Mkuu wa Mipango Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Pancras Bujuw  wakikata utepe kuashiria  umezindua wa  kituo cha computer katika Taasisi ya Taaluma za Maendeleo  Chuo Kikuu cha Dar es Salam.
 Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al-Najem   (alieekaa)   akifafanua jambo mara baada ya uzinduzi huo.
Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al-Najem akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa  Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo mara baada ya kuzindua kituo cha Kompyuta.
 
UBALOZI wa Kuwait nchini Tanzania umeanzisha mradi uitwao ““KITUO CHA KOMPYUTA KATIKA KILA TAASISI YA ELIMU” ambapo umezindua kituo cha Kompyuta katika Taasisi ya Taaluma za Maendeleo – Chuo Kikuu cha Dar es Salam. Hafla ya uzinduzi wa kituo hicho ambacho ni cha kwanza  ilihudhuriwa na Mkuu wa Taasisi hiyo Profesa Ester Dugumaro, Mkuu wa Uwekezaji na Mipango wa UDSM Dr. Bujuluru   pamoja na baadhi ya waalimu chuoni hapo.

Katika hotuba yake Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al-Najem alisisitiza kuwa Mradi Mpya unaolenga kuanzisha chumba cha Kompyuta katika taasisi za elimu ya juu ni muitikio wa wito uliotolewa na viongozi mbali mbali nchini  kuhusiana na kuweka mkazo katika kuinua elimu na kuunga mkono juhudi za Raisi John Magufuli aliyetangaza kutoa elimu bure kwa wananchi wote.

Balozi Al-Najem aliongeza kuwa mradi huu una lengo la kuanzisha idadi kubwa zaidi ya vituo vya Kompyuta katika vyuo mbalimbali nchini kote kwa kushirikiana na Asasi na Jumuiya za misaada za Kuwait na Tanzania, na hii ni kutokana na umuhimu  wa elimu kwa njia ya mtandao, Al-Najem aliongeza kuwa Chuo Kikuu cha Dodoma kitakua ndio kituo cha pili kufaidika na mradi huuu mkubwa, kikifuatiwa na  chuo kikuu cha Zanzibar (SUZA).

Kwa upande wake Profesa Ester Dugumaro alitoa shukurani za dhati kwa Nchi ya kuwait kwa niaba ya uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa misaada mbali mbali inayotolewa kwa Tanzania katika sekta ya elimu, huku akielezea matumaini yake ya kutiwa saini kwa makubaliano ya kushirikiana na Chuo Kikuu cha Kuwait  na vyuo vyengine nchini humo katika nyanja zote.

Bi. Dogomaro aliongeza kuwa wanafunzi wa Uzamili na Uzamifu ndio watakaofaidika zaidi na kituo cha kompyuta kilichoanzishwa na Ubalozi wa Kuwait   ambapo wataweza kutumia mitandao kutafuta taarifa na maelezo kwa madhumuni ya utafiti.

Yafaa kuweka wazi kuwa Ubalozi wa Kuwaiti hapa Tanzania umeanzisha miradi mbalimbali  katika kipindi cha hivi karibuni kama “Kisima cha Maji kwa Kila Shule” na “Maabara ya sayansi kwa kila shule” yenye lngo la kuisaidia Tanzania katika sekta ya elimu.  

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad