HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 23, 2017

DK. SHEIN: SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR HAITOMBAGUA MTU YOYOTE.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kutoa huduma zote muhimu kwa wananchi wake zikiwemo huduma za afya bila ya ubaguzi.

Dk. Shein aliyasema hayo leo, huko Junguni, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba mara baada ya kuzindua Kituo cha Afya cha Mama na Mtoto, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake kiswani Pemba.

Katika maelezo yake Dk. Shein alisema kuwa kamwe Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haitombagua mtu yoyote kwa itikadi yake ya kisiasa na badala yake itahakikisha wananchi wote Zanzibar wanapata huduma muhimu za maendeleo.

Dk. Shein alisema kuwa mwananchi yeyote anaekwenda kituoni hapo kupata huduma za afya hatabaguliwa kwani yeye ni mwananchi wa Zanzibar na akiwa mzazi atazalishwa kwa kufuata taratibu zote kwa mujibu wa taaluma aliyosomeshwa na Serikali.

Aidha, Dk. Shein alieleza kuwa iwapo mwananchi atajibagua mwenyewe kwa kutokwenda kituoni hapo kupata huduma hiyo itakuwa si lawama kwa Serikali kwani juhudi kubwa zimekuwa zikichukuliwa na Stikali ili wnannchi wote wapate huduma muhimu bila ya ubaguzi.

Aliongeza kuwa chama chochote duniani kinachoongoza nchi kikipeleka maendeleo basi hakiwakusidi wanachama wake pekee bali huwakusudia wananchi wote.

Pamoja na hayo Dk. Shein alilihakikishia Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia idadi ya Watu Duniani (UNFPA) kuwa Serikali ya Mainduzi ya Zanzibar inatambua wajibu wake na imo katika kutekeleza wajibu huo ambao umeelekezwa tokea wakati wa ASP mbapo katika Ilani yake ilielekeza hivyo.

Alisema kuwa Setikali haiwezei kuepuka wajibu wake katika kuwapelekea huduma muhimu wananchi wake lakini kinachokwamisha ni uhaba wa nyenzo na fedha lakini hata hivyo juhudi za makusudi huchukuliwa ili kuhakikisha mafanikiio yanapatikana.

Pia, Dk. Shein aliwataka akina baba kuwapa moyo wake zao wakati wanapokuwa wajawazito hata pale wanapojifungua kuwa nao karibu huku akieleza azma ya Serikali katika kuhakikisha vifo vya akina mama wajazito vinapungua kwa kiasi kikubwa.

Dk. Shein aliwahakikishia wananchi kuwa huduma za afya zitaendelea kuwa bure hasa kwa akina mama wajawazito ila pale panopotokea upungufu wa vifaa kuna haja ya kuchangia huku akitoa maagizo ya kupelekwa ultrasound pamoja na wafanyakazi ili kuondoa changamoto ya wafanyakazi kituoni hapo.

Sambamba na hayo, Dk. Sgein alitumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa Shirika la UNFPA kwa kuendelea kuisaidia Zanzibar kwani juhudi hizo zimeanzwa kuchukuliwa kipindi kirefu na Shirika hilo na Serikali itaendelea kufanya kazi pamoja na kushirikiana nalo.

Nae Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman alieleza kuwa katika kutoa huduma za afya hakuna haja ya ubaguzi na wafanyakazi wote wa Wizara hiyo wakiwemo wafanyakazi wa kituo hicho wamekuwa wakitoa huduma zao bila ya ubaguzi kama.

Naibu Waziri huyo alieleza kuwa wananchi wa Njuguni wamekuwa wakitoa mashirikiano makubwa kwa kutambua kuwa maendeleo hayana ubaguzi.

Mapema Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Asha Abdalla alieleza kuwa ujenzi wa kituo hicho cha afya umefanyika chini ya Mradi wa Afya bora unaofadhiliwa na Serikali ya Canada kupitia Shirika la kuhudumia watoto UNICEF na Shirika la Idadi ya watu Duniani UNFPA.

Alisema kuwa lengo kuu la mradi huo ni kuimarisha afya ya mama na motto kupitia uimarishaji wa miundombinu ya afya na uzazi na kuhakikisha upatikanaji wa huduma za dharura wakati na baada ya kujifungua.

Aliongeza kuwa jumla ya vituo sita katika ujenzi huo unaojumuisha utanuzi wa wodi za uzazi katika vituo hiyo na kusaidia upatikanaji wa vifaa muhimu katika utoaji wa huduma za uzazi ambapovituo viliomo katika mradi huo ni Junguni, Bogoa na Uondwe kwa Pemba na Fuoni, Sebleni na Tumbatu kwa Unguja.

Aidha, alisema kuwa ujenzi wa kituo hicho cha afya cha mama na motto umegharimu kiasi cha TZS milioni 165.8 pamoja na vifaa vyenye thamani ya TZS 107 ambapo kituo hicho kinahudumia watu 5,074 wa vijiji 16.

Nae Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Idadi ya Watu Duniani UNFPA nchini Tanzania Dk. Hashina Begum alisema kuwa lengo kubwa la misaada inayotolewa na Shirika hilo ni kuimaisha mifumo ya afya iliiweze kutoa kwa usawa huduma jumuishi za kiafya.

Pamoja na kuimaisha huduma za rufaa na kuongeza ubora katika kufikia na kutoa huduma za dharura za uzazi kwa mama, huduma za watoto wachanga pamoja na huduma za afya kwa wavulana na wasichana.

Alieleza kuwa lengo kubwa la Mradi huo ambao unajulikana pia kama ‘ Afya Bora ya Mama na Mtoto’ ni kuimarisha afya na ustawi wa mama, wavulana, wasichana na watoto hapa Zanzibar huku akiahidi kuwa Shirika hilo litaendelea kuiunga mkono Zanzibar.

 Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad