HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 23, 2017

SHANGWE NA VIGEREGERE MBEYA KWA WAHANGA WA SOKO LA SIDO KURUHUSIWA KUJENGA VYUMBA VYA BIASHARA VYA KUDUMU KATIKA MPANGILIO MAALUM ENEO LILILOTEKETEA KWA MOTO...

Baadhi ya wafanyabishara wa soko la Sido lililoteketea kwa moto hivi karibuni wakiwa wamebadirisha nyuso zao kutoka kwenye huzuni waliyokuwanayo baada ya kuteketea kwa vibanda vyao vya biashara, Serikali mkoani Mbeya imeridhia wahanga wa moto katika soko la sido kuendelea kubaki katika maeneo yao ya awali na kuagiza  wajenge vyumba vya kudumu ili kukabilina na majanga ya moto yanapojitokeza.
Akitoa maelekezo ya serikali mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla amewaagiza watendaji wa halmashauri kupiga kambi katika eneo la soko la Sido haraka kuanzia siku ya kesho kwa ajili ya kubuni michoro na mpangilio wa soko hilo ili wafanyabiashara waanze ujenzi.
Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa wilaya Ya Mbeya Mjini,mkoa ikiwa ni Pamoja na mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini Mh.Joseph Mbilinyi pamija na Naibu spika Bi.Tulia Akson ambaye ametoa msaada wa shilingi milioni 10 kwa wahanga hao.
 Aidha baada ya kutolewa kwa kiasi hicho mkutano huo umeridhia fedha hiyo ibaki na mkuu wa mkoa huku uongozi wa soko ukipanga matumizi ya fedha hiyo.
Hata hivyo mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh.Makalla ameliagiza jeshi la zimamoto kuendelea kutoa elimu ya zimamoto,kusambaza vithibiti moto na kuchimba visima vya maji vya ziada katika masoko huku akiwataka viongozi wa ngazi zote za mkoa kuchukua tahadhari za moto kwenye masoko kutokana na ripoti kuonesha chanzo cha janga hilo ni mabaki ya moto uliotokea kwenye moja ya vibanda vya mamalishe waliokuwa ndani ya soko hilo.
Viongozi mbalimbali wa Serikali, waandishi wa habari, wanasiasa pamoja na jeshi la polisi wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa mbeya Mh.Amos Makalla wakitembelea eneo la soko la Sido lililoteketea Kwa Moto hivi karibuni Jijini Mbeya.
PICHA ZOTE NA FADHIL ATICK MR.PENGO MBEYA.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh.Amos G. Makalla akizungumza na wahanga wa Soko la sido pamoja na wananchi walio hudhuria Mkutano huo ulio fanyika hii leo eneo la Sido Jijini Mbeya.

Naibu spika Bi.Tulia Akson akitoa pole kwa wahanga wa soko la sido pamoja na kuwasilisha pole yake ya Pesa Taslimu shilingi milioni 10 kwa wahanga hao


Mbunge wa jimbo la mbeya mjini Mh.Joseph Mbilinyi akiongea na wahanga wa Sido hawapo Pichani..

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad