
RC Makonda aagiza CV za watendaji kata za jiji la Dar es Salaam kupitiwa upya hatua hiyo imefuata baada ya Mkuu huyo wa Mkoa D ar es Salaam kufika
katika eneo la Bunju B jijini humo kwa maelekezo ya Rais Magufuli aliyetoa siku
4 kutatuliwa kero za eneo hilo.
Katika mkutano na wananchi wa eneo hilo, RC Makonda
alilazimika kumuinua mtendaji wa kata hiyo na ndipo alipogundua wengi wao
hawaelewi vizuri majukumu yao na ndipo alipomuagiza Mkuu wa Wilaya ya
Kindondoni, Ally Happi kukagua CV za watendaji wake mara moja.
RC Makonda amedai Watendaji hao kutoelewa majukumu yao ndio
imekuwa sababu kubwa ya wananchi kushindwa kutatuliwa kero ndogondogo na
hatimaye Wanasubiri Rais akipita wanamsimamisha kwa matatizo madogodogo
yakiwemo ya Vyoo, Umeme na masoko.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
akizungumza na wananchi wa Bunju B juu ya Watendaji
wa Kata kutoelewa majukumu yao imekuwa ni sababu
kubwa ya wananchi kushindwa kutatuliwa kero zao.
Sehemu ya wanchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar
es Salaam, Paul Makonda.
Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya jamii.
No comments:
Post a Comment