HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 9 August 2017

MCHENGA VS TMT NI FAINALI YA KWANZA KUMJUA MBABE WA SPRITE BBALL KINGS

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Michuano ya mpira wa kikapu ya Sprite BBall Kings 2017 imezidi kupamba moto baada ya timu zilizofanikiwa kuingia hatua ya fainali   kutambiana.

Michuano hiyo itakayoendelea wikiendi hii katika Viwanja vya Don Bosco imekuwa ya ushindani mkubwa ikiwa ni mchezo wa raundi ya kwanza hatua ya fainali.

Manahodha kutoka timu hizo wametambiana kwa kila mmoja kumuambia mpinzani wake kuwa ajipange katika mchezo huo wa raundi ya kwanza  katika kushindania lile taji la Sprite BBall kings ili kumpata mfalme wa kikapu kwa mwaka 2017.

Kwa upande wa timu ya mpira wa kikapu ya Mchenga Bball Stars, nahodha wao Mohamed Yusuph amesema kuwa watahakikisha mchezo wa raundi ya kwanza dhidi ya wapinzani wao TMT unamalizika Kwa wao kuwapiga vikapu vya kutosha wapinzani wao.

Nahodha wa TMT Isihaka Mzinga  ametamba na kuwatahadharisha Mchenga kuwa wajipange vyema, kwani kwa mchezo wa kwanza tu watahakikisha wanaonyesha uwezo wao wa kuibuka wafalme wa kikapu katika  Mashindano ya Sprite BBall kings 2017.

Mchezo wa kwanza wa Sprite BBall kings 2017, utachezwa katika viwanja vya Don Bosco Oysterbay na mshindi wa kwanza wa mashindano haya ataondoka na kitita cha shilingi milioni 10 ,mshindi wa pili milioni 3, na mchezaji bora milioni 2.
Sprite BBall kings 2017, ni kwa udhamini mkubwa kabisa wa kinywaji cha Sprite.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad