HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 9, 2017

• JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAENDELEA KUCHUNGUZA CHANZO CHA VURUGU ZILIZOTOKEA MTAA WA MABATINI WILAYANI NYAMAGANA.


•    JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAENDELEA KUCHUNGUZA CHANZO CHA VURUGU ZILIZOTOKEA MTAA WA MABATINI WILAYANI NYAMAGANA.

KWAMBA TAREHE 08.08.2017 MAJIRA Y A SAA 22:00 USIKU KATIKA MTAA WA MABATINI KATA YA MABATINI WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, GARI NAMBA T.394 DJW AINA YA TOYOTA HAICE AMBALO LINADAIWA LILIKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA ALIYEJULIKANA KWA JINA LA AMINI SHABANI SIZYA MIAKA 28, MNYAMWEZI, MKAZI WA MTAA WA MABATINI. INASEMEKANA KUWA DEREVA WA GARI HILO  WAKATI ALIPOKUWA MAHALI HAPO ALIGEUZA GARI LAKINI ENEO LILIKUWA FINYU HIVYO ALIKWENDA KUGONGA NYUMBA (PUB) ILIYOKUWA PEMBENI  MALI YA BONIFACE NTOBI NA KUVUNJA UKUTA NA KUSABABISHA UHARIBIFU WA MALI NA VITU VYENYE KIASI CHA THAMANI YA TSH 4,000,000/=.

INASEMEKANA KUWA BAADA YA TUKIO HILO KUTOKEA WANANCHI WALITOA TAARIFA KITUO CHA POLISI, ASKARI WALIFANYA UFUATILIAJI WA HARAKA HADI ENEO LA TUKIO NA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI NA KUFANIKIWA KUMKAMATA DEREVA WA GARI HILO, LAKINI IKATOKEA KUTOELEWANA KATI YA ASKARI WENGINE WALIOFIKA ENEO HILO NA MWENYE NYUMBA (PUB) PAMOJA NA WANANCHI NA KUPELEKEA KUZUKA KWA VURUGU AMBAPO WANANCHI WALIANZA KUWARUSHIA ASKARI MAWE NDIPO ASKARI WALIFYATUA RISASI KADHAA HEWANI  HALI ILIYOPELEKEA HOFU  KWA WANANCHI WA ENEO HILO.

KATIKA VURUGU HIZO MKE WA MWENYE NYUMBA (PUB) BI BETI ATANASI ALIJERUHIWA MGUU WA KULIA JUU YA UNYAYO, LAKINI BADO HAIJATHIBITIKA KUWA JERAHA HILO NI LA KITU GANI KWANI MAJERUHI ANAONGEA NA ANAWEZA KUTEMBEA YUPO HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU HIVYO TUNASUBIRI UCHUNGUZI WA KISAYANSI WA DAKTARI ILI KUWEZA KUTHIBITISHA JUU YA JERAHA HILO.

AIDHA KUFUATIA VURUGU ZILIZOTOKEA KATIKA ENEO HILO NA KUSABABISHA ASKARI KUFYATUA RISASI. JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LIMEANZA UCHUNGUZI WA SUALA HILO ILI KUBAINI CHANZO HALISI CHA VURUGU HIZO.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA, AKIWATAKA KUTULIA WAKATI JESHI LIKIENDELEA NA UCHUGUZI KUHUSIANA NA TUKIO HILO. AIDHA PIA ANAWAOMBA WANANCHI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI ILI LIWEZE KUENDELEA KULINDA USALAMA WA RAIA PAMOJA NA MALI ZAO KATIKA MKOA WETU WA MWANZA.

IMETOLEWA NA;
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad