HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 7 August 2017

Kesi ya kumtukana Rais inayomkabili Mdee, yapigwa kalenda.

Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeahirisha kesi ya kutoa lugha chafu dhidi ya Rais John Pombe Magufuli inayomkabili mbunge wa Kawe, Halima Mdee hadi Septemba 12, kwa kuwa hakimu anayesikiliza kesi hiyo anaudhuru.

Hata hivyo, kabla ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, Mshtakiwa Mdee  kupitia mawakili wake amewasilisha pingamizi la awali katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwamba mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

Mawakili wa Mdee, wakiongozwa na Hekima Mwesigwa wamewasilisha pingamizi hilo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa baada ya wakili wa serikali Leonard Chalo kudai shauri hilo limekuja kwa ajili ya kutajwa.

Mwesigwa amedai kuwa wanapingamizi mbili, kwanza hati ya mashtaka ina mapungufu, pia Mahakama hiyo haina mamlaka.

Amedai kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka kwa sababu, Mkuu wa wilaya aliyetoa amri ya kukamatwa kwa Mdee ameshindwa kufuata matakwa ya kisheria.

Hata hivyo, Hakimu Mwambapa hakujibu kitu chochote na ameiahirisha kesi     hiyo hadi September 12 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad