HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 7 August 2017

Kesi ya Kaburu na Aveva, Upelelezi bado haujakamilika

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeiharisha Kesi ya utakatishaji fedha inayomkabili Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange maarufu Kaburu hadi August 16 mwaka 2017 kwa sababu upelelezi haujakamilika.

Kesi hiyo ilitajwa leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa na wakili wa serikali, Elia Athanas ambaye amedai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, hivyo anaomba ipangiwe tarehe nyingine.

Hakimu Mwambapa alikubali maombi ya wakili wa Serikali Athanas na  aliahirsha kesi hiyo hadi August 16 mwaka huu.Kesi ya Kaburu na Aveva, Upelelezi bado haujakamilika

Aveva na Kaburu wamerudishwa tena mahabusu mpaka kesi yao itakapotajwa tena.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad