Mtaa Kwa Mtaa Blog

HOTEL 92 ILIYOPO SINZA SHEKILANGO ROAD NA MADUKA YABOMOLEWA KWA AMRI YA MAHAKAMA

Jengo  la iliyokuwa hotel 92 Sinza Shekilango jijini Dar es salaam ambalo linatumika kama kanisa na maduka  plot namba 11 limevunjwa na kampuni ya CEMINA AUCTIONAL MART ikiwa ni utekelezaji wa hukumu ya Mahakama kuu kitengo cha Ardhi baada ya aliyekuwa mmiliki wa eneo hilo  NKUMILO ENTERPRESES kushindwa kesi mahakamani.

ITV imefika katika eneo hilo na kukuta shughuli za uvunjaji zikiendelea katika ploti hiyo iliyokuwa na maduka pamoja ukumbi ambao ulikuwa ukitumiwa na waumini wa kanisa la SHALOM TABERNACLE INTERNATIONAL CHURCH ambapo waumini walionekana wakihaha kutoa mali za kanisa hilo.

Akizungumza na radio one mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya CEMINA AUCTIONAL BI ROSE JOSEPH amesema wamepewa jukumu hiyo na mahakahama baada ya kesi ya ploti hiyo iliyodumu kwa miaka minne kumalizika na kumpa ushindi aliyenunua eneo hilo Bw. Yusuph Ismail

Wafanyabiashara waliokuwa na maduka katika ploti hiyo wamesema kwa sasa hawana cha kufanya kwani awali hawakaumbiwa kama eneo hilo linamgogoro .

Chanzo: ITV Tanzania
Labels:

Post a Comment

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget