HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, August 29, 2017

NGAO YA JAMII MPYA YA SIMBA IKO TAYARI, SASA KUKABIDHIWA RASMI SEPT 06


Afisa habari wa TFF Alfred Lucas akionesha Ngao ya Jami mpya iliyofanyiwa marekebisho na tayari kukabidhiwa kwa Klabu ya Simba  siku ya mechi ya ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Azam FC.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

BAADA ya kufanyika kwa makosa wakati wa utengenezaji wa Ngao ya Jamii, Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini 'TFF'  imetengeneza Ngao mpya kwa ajili ya klabu ya Simba baada ya ile ya awali kukosewa kuandikwa.


Klabu ya Simba ilifanikiwa kushinda katika mchezo wa Ngao ya Jamii August 23, 2017 baada ya kuifunga kwa mikwaju ya penati 5-4 mahasimu wao Yanga na kukabidhiwa Ngao ya Jamii ambayo ilikuwa na makosa ya kiuandishi.


Ngao ya Jamii ya awali iliyokabidhiwa kwa washindi hao wa mwaka 2017 Simba iliandikwa ‘Community Sheild’ badala ya ‘Community Shield’ kitu ambacho kilizua mijadala kwenye mitandao ya kijamii na kupelekea TFF kuomba radhi kwa wanafamilia wa mpira wa miguu nchini na kuahidi tukio kama hilo halitojirudia tena.

Afisa habari wa TFF Alfred Lucas ameionesha Ngao ya Jamii iliyofanyiwa marekebisho itakabidhiwa  kwa Simba siku ya mechi ya ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Azam FC.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad