HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 29 August 2017

Balozi Asha-Rose Migiro awatembelea Watanzania waishio Birmingham

Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mheshimiwa Asha-Rose Migiro alifanya ziara ya kuwatemebelea Watanzania waishio katika mji wa Bimingham na vitongoji vyake tarehe 28/8/2017.

Pamoja na ziara hiyo, Mhe. Balozi Migiro alipata nafasi ya kushiriki katika uzinduzi rasmi wa Jumuiya ya Watanzania waishio katika mji huo wa Birmingham na Vitongoji vyake, ijulikanayo kama Watanzania wa Birmingham na nchi nyeusi -(Tanzanian's in Birmingham and Black Country - WBBC).

Mhe. Balozi aliwapongeza na kutoa wito kwa  Watanzania hao kuwa na kushirikiano wa karibu na Ofisi za Ubalozi kupitia Viongozi wao. Pia alihimiza umuhimu wa Wana diaspora kuwa wamoja na kushirikiana bila kubaguana.

Katika Mkutano huo, kulifanyika hafla ndogo ya kuchangia Jumuiya hiyo pamoja na chakula cha pamoja kwa kumshukuru Mhe.Balozi kwa kutenga muda wake na kuwatembelea.

Sambamba na hafla hiyo Mheshimiwa Balozi Asha-Rose Migiro pia alizindua rasmi Jumuiya hiyo, na kukabidhiwa Katiba yao itakayo tumika kuendesha shughuli za kila siku za Jumuiya hiyo.

 Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Balozi Migiro akiwahutubia Watanzania waliohudhuria katika mkutano huo kushoto kwake ni katibu wa Jumuiya ya Watanzania waishio Birmingham na Black Country Dkt. Hassan Khalfan Hamidu, anayefuatia ni Mbunge kutoka jimbo la Stafford wa chama cha Conservative Jeremy John Lefroy na nyuma ya Balozi ni Mwambata wa Uhamiaji Ubalozini Bw. Magnus Ulungi.
 Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Balozi akiwa na viongozi wa Jumuiya ya Watanzania waishio Birmingham Mwenyekiti wa WBBC Bw. Renatus Mgetta(Pili kulia), Katibu wa Baraza la Ushauri Brian M. Ngelangela.; Kutoka kushoto mwa picha ni Katibu Mwenenzi Dr. Dr. Othman M., Katibu wa Jumuiya Dr. Hassan Khalfan na Kiongozi wa Kamati ya Katiba, Uratibu na Mwongozo Bw. Nelson Kampa.
 Mbunge kutoka jimbo la Stafford wa chama cha Conservative Jeremy John Lefroy akihutubuia katika mkutano huo wa wanadispora.
 Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Balozi Migiro akijumuika na watanzania katika kucheza muziki
 Balozi Asha-Rose Migiro akizungumza na Mwenyekiti wa British Tanzania Society (BTS) Prof. Andrew Coulson wakati wa mkutano huo.
Mheshimiwa Balozi, akijumuhika na Watanzania hao katika chakula cha pamoja

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad