 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kati kati akisalimiana na Mwakilishi wa Taasisi ya Kimataifa ya kujitolea inayojishughulisha na masuala ya Kibinaadamu ya Umoja wa Falme za Kiarabu {UAE } ya Emirates Red Crecent Bwana Said Al – Khemeir. Wa kwanza kutoka Kulia ni Mhandisi wa Taasisi ya Emirates Red Crecent Bwana Fateh Basel.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kati kati akisalimiana na Mwakilishi wa Taasisi ya Kimataifa ya kujitolea inayojishughulisha na masuala ya Kibinaadamu ya Umoja wa Falme za Kiarabu {UAE } ya Emirates Red Crecent Bwana Said Al – Khemeir. Wa kwanza kutoka Kulia ni Mhandisi wa Taasisi ya Emirates Red Crecent Bwana Fateh Basel. Balozi Seif akizungumza na Ujumbe wa Viongozi wa Taasisi ya Kimataifa ya kujitolea inayojishughulisha na masuala ya Kibinaadamu ya Umoja wa Falme za Kiarabu {UAE } ya Emirates Red Crecent Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Balozi Seif akizungumza na Ujumbe wa Viongozi wa Taasisi ya Kimataifa ya kujitolea inayojishughulisha na masuala ya Kibinaadamu ya Umoja wa Falme za Kiarabu {UAE } ya Emirates Red Crecent Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Taasisi
 ya Kimataifa ya kujitolea inayojishughulisha na masuala ya Kibinaadamu 
ya Umoja wa Falme za Kiarabu {UAE } inakusudia kujenga Nyumba  Mpya  za 
Kisasa za Makaazi  katika Wilaya tofauti za Zanzibar kwa  ajili ya  
Wananchi ambao Nyumba zao zimekumbwa na Maafa wakati wa msimu wa Mvua za
 Masika uliopita.
Ujenzi
 wa nyumba hizo unafuatia wito wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  wa 
kuzitaka Nchi, Taasisi na Mashirika rafiki  ndani na nje ya Nchi 
kusaidia kuunga mkono Wananchi walioathirika na Mvua hizo ambao wengine 
wamepoteza kabisa Makaazi yao.
Mwakilishi wa Taasisi ya Kimataifa
 ya kujitolea inayojishughulisha na masuala ya Kibinaadamu ya Umoja wa 
Falme za Kiarabu {UAE } ya Emirates Red Crecent Bwana Said Al – Khemeir 
alitoa kauli hiyo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa
 Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar.
Bwana Said 
alisema Uongozi wa Taasisi yake ulifika Zanzibar kuangalia maeneo 
yaliyoathirika na Mvua hizo na kuandaa Mipango itakayosaidia kuanzwa kwa
 Mradi huo mkubwa utakaohusisha Wilaya zote zilizopatwa maafa hayo.
Alisema
 Awamu ya kwanza ya mradi huo itaanza Kisiwani Pemba kwa ujenzi wa 
Nyumba 30, zitakazokuwa na uwezo wa kuchukuwa Familia Mbili, Skuli yenye
 Madarasa Saba na Maktaba yake, Hospitali, Msikiti pamoja na Maduka kwa 
ajili ya wakaazi watakaoishi eneo husika.
Mwakilishi huyo  wa 
Taasisi ya Kimataifa ya kujitolea inayojishughulisha na masuala ya 
Kibinaadamu ya Emirates Red Crecent alisema Taasisi hiyo yenye kufanya 
kazi chini ya ushauri wa Vyama vya Msalaba  Mwekundu na Mwezi Mwekundu 
Duniani imekuwa ikitoa huduma za kibinaadamu katika Mataifa mbali mbali 
Duniani kutegemea na mahitaji ya Nchi husika.
Naye Mhandisi 
Muandamizi wa Taasisi hiyo ya Emirates Red Crecent Fateh Basel 
aliishauri Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwamba maeneo 
yatakayotengwa kwa ajili ya ujenzi wa Nyumba hizo ni vyema yakawa 
salama.
Mhandisi Basel alisema maeneo yatakayotengwa endapo 
yatakuwa  karibu na miundombinu ya Bara bara, Maji na Huduma za Umeme 
yatasaidia kurahisisha mradi huo kukamilika kwa haraka ili kutoa faraja 
kwa Wananchi waliothirika na Mvua za masika zilizopita.
Aliupongeza
 ushirikiano wa karibu ulioonyeshwa na watendaji wa Wilaya na Mikoa 
wakati wa ziara yao ya kukagua sehemu zilizoathirika na Mvua za Masika 
pamoja na kuangalia baadhi ya maeneo salama yenye sifa na haiba ya 
kujengwa kwa mradi huo.
Akitoa shukrani zake  kwa Uongozi wa 
Taasisi hiyo ya Emirates Red Crecent Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar 
Balozi Seif Ali Iddi alisema kitendo kilichobuniwa na Taasisi hiyo 
hakitolea faraja kwa Wananchi walioathirika na janga hilo pekee bali 
hata na Serikali Kuu kwa ujumla.
Balozi Seif alisema atauagiza 
Uongozi wa Kila Mkoa na Wilaya Visiwani Zanzibar kufanya utafiti na  
uhakiki wa kuangalia maeneo yatakayoweza kuanzishwa miradi hiyo 
itakayostawisha Wananchi waliokusudiwa.
Makamu wa Pili wa Rais wa
 Zanzibar aliuhakikishia Uongozi huo wa Emirates Red Scecent kwamba 
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itazingatia wazo hilo kwa ajili ya 
kulitolea baraka zake ili Mradi huo uanze mara moja na kulet tija 
iliyokusudiwa. 
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
21/7/2017.
 Mwakilishi wa Taasisi ya Emirates Red Crecent ya Umoja wa Falme za Kiarabu Bwana Said Al – Khemeir wa Pili kutoka Kushoto akimfafanua Balozi Seif nia ya Taasisi yake kujenga  Nyumba kwa ajili ya Wananchi walioathirika nja Mvua za Masika.
 Mwakilishi wa Taasisi ya Emirates Red Crecent ya Umoja wa Falme za Kiarabu Bwana Said Al – Khemeir wa Pili kutoka Kushoto akimfafanua Balozi Seif nia ya Taasisi yake kujenga  Nyumba kwa ajili ya Wananchi walioathirika nja Mvua za Masika. Mhandisi wa Taasisi ya Milele Zanzibar Foundation  Bwana Khamis Rasshid wa kwanza kutoka Kulia ambaye Kampuni yake ndio itakayosimamia Ujenzi wa Nyumba za Wananchi walioathirika na Mvua za Masika akifafanua jambo wakati Ujumbe wa Emirates Red Crecent upofanya mazunguma na Balozi Seif.
 Mhandisi wa Taasisi ya Milele Zanzibar Foundation  Bwana Khamis Rasshid wa kwanza kutoka Kulia ambaye Kampuni yake ndio itakayosimamia Ujenzi wa Nyumba za Wananchi walioathirika na Mvua za Masika akifafanua jambo wakati Ujumbe wa Emirates Red Crecent upofanya mazunguma na Balozi Seif. 

 
 


 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment