Balozi huyo alikutana na Makamu wa 
Rais na kumuaga rasmi kwani muda wake wa kutumikia nchini ulikuwa 
umemalizika. akamu wa Rais alisema anafurahi kuona Idadi kubwa ya 
Watalii kutoka Israel wanaokuja Tanzania. 
“Tunawakaribisha sana Tanzania, waje kwa wingi wao, tunawakaribisha kwa mikono miwili” na alimuhakikishia Balozi huyo kuwa Tanzania itaendelea kuimarisha  mahusiano yaliyopo baina ya nchi hizi mbili. 
Kwa
 upande wake Balozi Yahel alisema watalii kutoka nchini Israel 
wameongezeka kutokana na kuvutiwa na mazingira mazuri , amani na utulivu
 wa nchi. 
Balozi Yahel alisema atakuwa mjumbe wa kuitangaza Tanzania popote duniani .

Makamu
 wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan 
akisalimiana na Balozi wa Israel nchini Mhe. Yahel Vilan (kushoto) 
ambaye muda wake wa kutumikia umemalizika na alifika kumuaga Mhe. Makamu
 wa Rais kwenye makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam kwa lengo la 
kuaga .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


Makamu
 wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan 
akizungumza na Balozi wa Israel nchini Mhe. Yahel Vilan (kushoto) ambaye
 muda wake wa kutumikia umemalizika na alifika kumuaga Mhe. Makamu wa 
Rais kwenye makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam kwa lengo la 
kuaga .

Makamu
 wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan 
akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Israel nchini Mhe. Yahel Vilan
 (kushoto)ambaye muda wake wa kutumikia umemalizika na alifika kumuaga 
Mhe. Makamu wa Rais kwenye makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam 
kwa lengo la kuaga . 
 

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment