HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 21, 2017

KOMBE LA MATAIFA AFRIKA SASA KUFANYIKA JUNI NA JULAI 2019 NCHINI CAMEROON


Shirikisho la soka barani Afrika  (CAF) limethibitisha.kuwa Kombe la mataifa bingwa Afrika 2019 litafanyika mwezi Juni na Julai 

Mchuano huo huwa unafanyika mnamo mwezi Januari na Februari na kusababisha migogro na vilabu vya Ulaya ambavyo hulazimika kuwatoa wachezaji katikati ya msimu.

Kinyang'anyiro hicho cha 2019 kitakachoandaliwa Cameroon kitashirikisha timu 24 badala ya 16. Mabadiliko hayo yalitiwa sahihi na kamati kuu ya CAF katika mkutano uliofanyika mji mkuu wa Rabat.

Michuano hiyo imekuwa ikishirikisha timu 16 tangu 1996. Upanuzi wa mechi hizo unaweza kusababisha matatizo kwa Cameroon ambayo itaanda fainali ijayo, huku waziri wa michezo wa taifa hilo la Afrika ya kati akilazimika kukataa ripoti kwamba maandalizi yalikuwa nyuma.

Mashindano hayo yataendelea kila baada ya miaka miwili barani Afrika. Caf ilikuwa inapanga iwapo itaruhusu mataifa kutoka mabara mengine kushiriki ama hata kuandaa mchuano huo.

Tangazo hilo linajiri kufuatia mkutano wa siku mbili ulioandaliwa na rais wa Caf Ahmad kuzungumzia hali ya soka barani Afrika.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad