HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 12 July 2017

RWANDAIR KUANZA SAFARI ZA BRUSSELS, UBELGIJI

Shirika la ndege la RwandAir linataraji kuanzisha safari zake za kuelekea mji wa Brussels nchini Belgium kupitia Mjini Kigali nchini Rwanda kutokea Jijini Dar es salaam.

akizungumzia kuanza kwa safari hizo, Meneja mkazi wa Shirika hilo, Ibrahim Bukenya amesema kuwa safari hizo zitaanza rasmi tarehe 14 Julai 2017 na zitakuwa ni safari za mara tatu kwa wiki na baadae kuwa kila siku. 

Bukenya amesema Shirika hilo liko kwenye hatua za mwisho kuweka Hub nyingine ya kibiashara kwenye mji wa Cotonou nchini Benin. Pia shirika hilo liko kwenye hatua za mwisho za kuanzisha safari zake mpya za kuelekea  mji wa Guangzhou nchini China.
Wakati huo huo shirika ndege la RwandAir kwa hapa Tanzania liko kwenye hatua za mwisho za kuanzisha malipo ya ununuzi wa tiketi kwa kutumia mitandao ya simu. 

Bukenya aliendelea kuwashukuru wateja wote na wadau wao na kwa kuwakumbusha kuwa safari zake kutokea Dar kuelekea Kigali na kuunganisha sehemu nyinginezo kuwa mara mbili kila siku, na kutokea Kilimanjaro kwenda Kigali na kuunganisha sehemu zingine ikiwa ni mara tano kwa wiki, hivyo kila atakaye kusafiri asafiri na Shirika ndege la RwandAir.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad