HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 6 July 2017

NSSF YAZINDUA MIKOPO KWA WANACHAMA WAKE KUPITIA BENKI YA AZANIA

Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) lazindua utoaji wa  mikopo  kwa  SACCOS na kupitia Benki ya Azania. Mikopo hii ni mahususi kwa ajili ya kuwasaidia wanachama wa NSSF kuweza kujikwamua kiuchumi hususan kuweza kutekeleza sera ya Viwanda ya awamu ya tano kwa kutumia mikopo hiyo kufungua Viwanda vidogo vidogo. 
Mikopo hiyo itatolewa hadi kiwango cha juu kisichozidi fedha taslimu za kitanzania  300,000,000 kwa SACCOS au AMCOS. Vile vile mwanachama wa NSSF anaweza kukopa hadi shilingi 20,000,000 kupitia SACCOS au AMCOS aliyojiunga nayo na mikopo hiyo italipwa ndani ya miezi 24
Alipokuwa akizindua mpango huo, Makamu wa Rais Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan aliwaasa wanachama wa NSSF kuchangamkia fursa hiyo ya mikopo na kuwaomba waitumie mikopo hiyo kama chachu ya kujikwamua kiuchumi na kuwaasa kuwa na nidhamu ya hali ya juu katika kuendeleza biashara zao.
Akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa mpango huo Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof Godius Kahyarara alisema SACCOS na AMCOS zote zitakaoomba mikopo hiyo ni lazima ziwasilishe  taarifa sahihi za fedha zilizokaguliwa  kwa miaka mitatu na kuhakikiwa na COASCO na mwanachama anaruhusiwa kukopa hadi mara tatu ya Amana zake alizijiwekea ndani ya SACCOS au AMCOS ambayo yeye ni mwanachama.
 Makamu wa Rais wa Jammhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.Mama Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Mikopo ya NSSF Kupitia Benki ya Azania alipotembelea banda la NSSF katika maonesho ya Sabasaba katika viwanja vya Mwalimu Nyerere.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mama Samia Suluhu Hassan  akipata maelezo kuhusu dawa  ya kuangamiza viuadudu vinavyosababisha ugonjwa wa malaria alipotembelea banda la NSSF katika maonesho ya Sabasaba, viwanja vya Mwalimu Nyerere. NSSF ni mdau wa kiwanda hicho cha Viuadudu kilichopo mkoani Pwani.
Mkurugenzi mkuu wa NSSF Prof. Godius Kahyarara akitoa ufafanuzi kuhusu mikopo ya NSSF kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe Mama Samia Suluhu Hassan kabla ya kuzindua rasmi mikopo hiyo katika viwanja vya Sabasaba.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad