HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 19 July 2017

MPAKANI YAKATA TIKETI YA ROBO FAINALI NDONDO CUP

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.TIMU ya Mpakani imefanikiwa kuingia katika hatua ya robo fainali baada ya kuwafunga mahasimu wao Makuburi kwa mikwahu ya penati 5-4.

Mchezo huo wa hatua ya 16 bora ya michuano ya Ndondo Cup inayoendelea katika Uwanja wa Kinesi, Sinza ulikuwa ni mchezo wa tatu wa hatuia hiyo baada ya timu ya Goms United kuanza kufungua milango ya kuingia hatua ya robo fainali kwa kuifunga Burudani. 

Mechi hiyo iliyokuwa ya ushindani iliweza kumalizika katika dakika 90 bila timu yoyote kuona mlango wa mwenzio na kwenda katika Mikwaju ya penati.
Beki kisiki wa timu ya Mpakani (jezi ya njano) Issa Rashid Baba Ubaya akiwania mpira na mchezaji wa Makuburi katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya michuano ya Ndondo Cup ambao ulimalizika kwa Mpakani kuibuka na ushindi wa penati 5-4.
Beki wa kushoto wa timu ya Makuburi Emmanuel Kichiba akiwa na mpira katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya michuano ya Ndondo Cup ambao ulimalizika kwa Mpakani kuibuka na ushindi wa penati 5-4.
Wachezaji wa timu ya Mpakani na Makuburi wakiwania mpira hewani katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya michuano ya Ndondo Cup ambao ulimalizika kwa Mpakani kuibuka na ushindi wa penati 5-4.
Manahodha wa timu ya Makuburi na Mpakani wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo wa hatua ya 16 bora ya michuano ya Ndondo Cup ambao ulimalizika kwa Mpakani kuibuka na ushindi wa penati 5-4.
Timu za Makuburi na Mpakani wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo wa hatua ya 16 bora ya michuano ya Ndondo Cup ambao ulimalizika kwa Mpakani kuibuka na ushindi wa penati 5-4.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad