HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 26, 2017

MAKONDA ATAKA NYUMBA ZA KULALA WAGENI PAMOJA NA KUMBI ZA STAREHE ZILIZO KARIBU NA MAENEO SHULE ZIVUNJWE

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewaagiza wakurugenzi wa Halmashauri katika jiji la Dar es Salaam ndani ya siku 20 kusiwepo nyumba za wageni pamoja na kumbi za starehe katika shule.
Makonda ameyasema hayo wakati akizungumza na wakuu wa shule za sekondari na Msingi. Makonda amesema kuwa  shule ni kwa ajili ya kutoa elimu hivyo kuwepo kwa vitu hivyo vinafanya kuhalibu wanafunzi.
Amesema kuwa maeneo yote ya shule yapimwe ili kusiwepo kwa mazingira ya kuweza watu kufanya kujenga maeneo hayo.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na maafisa elimu, waalimu wakuu shule za sekondari na msingi uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa akizungumza na katika Mkutano wa Walimu Wakuu Shule za Sekondari na Msingi uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Shule Kisarawe 11,  Elieshi Emmanuel akizungumza katika Mkutano wa Wakuu wa Shule juu uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya walimu wakuu wakiwa kwenye mmkutano na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam leo. 

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwasikiliza walimu wakuu wa msingi pamoja na sekondari walipokuwa wanawasilisha maoni yao leo kwenye mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya jamii

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad