HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 26 July 2017

MAGONJWA YASIOAMBUKIZWA YANAWEZA KUEPUKIKA KWA KULA VYAKULA VYA ASILI PAMOJA NA KUFANYA MAZOEZI

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Magonjwa yasioambukizwa yanaweza  kuepukika kutumia vyakula vya asili pamoja na kufanya mazoezi ambapo hakuna gharama inaweza kufanya mtu kuchangia.
Magonjwa hayo ni Kisukari, shinikizo la Damu, pamoja na Unene wa kupindukia
Hayo aliyasema Mwenyekiti wa Kikundi cha Mtambani  kilichopo Mlandizi wilayani Kibaha, mkoani Pwani, Mohamed Pongwe wakati akizungumza na Michuzi Blog, amesema kuwa magonjwa yasiombukizwa yanaweza kuepukika kwa kula vyakula visivyo na mafuta pamoja na kufanya mazoezi katika mazingira wanayoishi.
Amesema walipata elimu baada ya Shirika la Help Age International  kupitia mradi wa Afya kwa Rika Zote  ambapo  waliweza kuanza ufugaji wa kuku pamoja na kilimo cha mboga mboga.
Pongwe amesema kuwa wanafanya kilimo cha mboga mboga  na ufugaji wa kuku  ambapo wanauza na fedha zinazopatika zinaingia katika kikundi pamoja na wao wenyewe kula mboga mboga na mayai na nyama za kuku hali ambayo imeweza kuboresha afya zao.
Mwanakikundi Mwajuma Fanuel amesema kuwa wameweza kuwa ni watu wanaojali afya kwa kula vizuri .
Amesema kuwa wakati wanafanya mradi huo Help Age International iliwasaidia mashine ya kusukuma maji katika kufanya umwagiliaji wa kilimo cha mbogamboga.
Aidha amesema katika miradi hiyo wameza kupata laki tano ambapo uzalishaji unaendelea katika maeneo yote ikiwa ni pamoja na kubadilika kiuchumi katika kikundi.
 Mwenyekiti wa Kikundi Cha Mtambani, Mohaamed Pongwe akizungumza na Michuzi Blog katika sehemu wanayofanya kilimo cha mboga mboga.
 Mwanakikundi, Mwajuma Fanuel akizungumza na Michuzi Blog katika sehemu ya kilimo cha mbogamboga .
 Baadhi ya wanakikundi wakiweka mbolea ya kinyesi cha kuku katika shamba la mbogamboga.
Wanakikundi wa Mtambani Mlandizi wakiwa katika picha ya pamoja 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad