HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 26 July 2017

MASHINDANO YA NDONDO CUP YAENDA RASMI MKOANI MWANZA

 Mratibu na muandaaji wa Michuano ya Sports Extra Ndondo Cup Shafii Dauda akimkabidhi Mkuu wa Mkoa John Mongela jezi ya Ndondo Cup ikiwa ni baada ya kuipelekea kwa mara ya kwanza nje ya Mkoa wa Dar es salaam na kupokelewa kwa shangwe na wananchi wa Mkoa huo.
Mratibu na muandaaji wa Michuano ya Sports Extra Ndondo Cup Shafii Dauda akimkabidhi Kamanda Maalum wa Polisi Mkoa wa  RPC Ahmed Msangi  jezi ya Ndondo Cup ikiwa ni baada ya kuipelekea kwa mara ya kwanza nje ya Mkoa wa Dar es salaam na kupokelewa kwa shangwe na wananchi wa Mkoa huo.


Baada ya kukabidhiwa jezi hizo na Mratibu na muandaaji wa Michuano ya Sports Extra Ndondo Cup Shafii Dauda ikiwa ni baada ya kuyapeleka rasmi mashindano hayo mkoani Mwanza, Mkuu wa Mkoa pamoja Kamanda Maalum wa Polisi Mkoa walikuwa na ya kusema.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela amesema kuwa licha ya kwamba sisi kuitaka Ndondo Cup kwa muda mrefu, tunaamini haijachelewa kuja Mwanza. Uwepo wa Ndondo Cup hapa ni fursa kwa vijana kwenye nyanja mbalimbali pamoja na moja kwa moja kukuza vipaji vya soka.

 Kamanda Maalum wa Polisi Mkoa wa  RPC Ahmed Msangi  amesema kuwa unaamini muda ambao Ndondo Cup inafanyika itawaleta vijana pamoja na kusaidia kupunguza vitendo vya kiharifu. Ni bora wakae makundi kwenye Ndondo Cup kuliko kukaa kwenye makundi mengine.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad