HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 14, 2017

HARBINDER SETHI ADAIWA KUWA NA UVIMBE TUMBONI, KESI YAKE YASHINDWA KUENDELEA YAPIGWA KALENDA

Na Karama Kenyunko,  
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeambiwa kuwa, mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Power African Power (T) Limited (PAP) ambaye pia ni mshitakiwa wa kwanza katika kesi ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha, Harbinder Singh Sethi ni mgonjwa sana na anasumbuliwa na uvimbe tumboni.

Taarifa hiyo imetolewa leo na Wakili wa mshitakiwa, Alexi Balomi  ambaye amedai mahakamani hapo kuwa, hali ya mteja wake Seth imekuwa ikibadilika kwa wiki nne sasa na kwamba imezidi kuwa mbaya kwa kuwa hawezi kupata usingizi na hivyo anahitaji uangalizi wa madaktari..

Kabla ya hoja hiyo ya ugonjwa, Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi Mwendesha Mashitaka Mwandamizi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai  alidai kuwa kesi hiyo ilikuja kwa kutajwa na upelelezi bado haujakamilika.

Balomi amedai kuwa kutokana na hali mbaya ya mteja wake Seth,wamebahatika  kupata nyaraka kadhaa kutoka kwa daktari kwani Hata siku aliyokamatwa alikuwa akienda kwenye matibabu Afrika Kusini alisema huku akitaka kutoa nyaraka hizo.

Hata hivyo, Swai  alidai nyaraka ambazo Wakili Balomi  anataka kuziwasilisha mahakamani  hapo  kuhusiana  na Sethi hazijakidhi vigezo vya sheria  na kwamba alitegemea daktari ambaye anamtibu angefika mahakamani kueleza hali  halisi ya ugonjwa husika.

 Akijibu hoja hiyo, Hakimu Shaidi amesema suala la ugonjwa siyo la kufumbiwa macho, linapaswa kuchukuliwa kwa uzito na kuelekeza magereza kufanya kila linalowezekana  kuhakikisha hali ya mshitakiwa huyo inakuwa nzuri na ikibidi, wawasiliane  na wataalam wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili kuhakikisha mshitakiwa anapohitajika mahakamani anafika kama inavyotakiwa.

Kesi imeahirishwa hadi Julai 28, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la.

 Seth anashtakiwa  pamoja na James Rugemarila ambaye ni Mkurugenzi wa VIP Engineering na mmiliki mwenza wa zamani wa Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Ltd (IPTL), ambao wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka  12 ya  uhujumu uchumi  kwa kuisababishia serikali hasara ya dola za Marekani milioni 22. 1 na Sh bilioni 309 pamoja na utakatishaji fedha.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad