HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 14, 2017

Wakulima wa Tumbaku waomba serikali kupambana na changamoto zinazoikumba sekta hiyo

Rais wa Chama cha Wakulima wa Tumbaku Duniani(ITGA), Daniel Green(wa pili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu mkutano unaoendelea wa kujadili changamoto zinazoikumba secta ya Tumbaku.Mazungumzo hayo yalifanyika katika Hoteli ya Lamada Dar es Salaam jana.Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Chama hicho(CEO), Antonio Abrunhosa na kutoka ktoka kulia ni Mtendaji Mkuu wa Chama cha Tumbaku Tanzania(FDTU), Miraji Mgalula na Mkurugenzi msaidizi wa Wizara ya Kilimo,Ufugaji na Uvuvi, Dk.Jackson Nkuba.
Mtendaji Mkuu wa Chama cha Wakulima Duniani(CEO), Antonio Abrunhosa (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu mkutano unaoendelea wa kujadili changamoto zinazoikumba secta ya Tumbaku unaofanyika katika Hoteli ya Lamada jijini Dar es Salaam.Kulia ni Rais wa Chama hicho, Daniel Green.
Mkurugenzi msaidizi wa Wizara ya Kilimo,Ufugaji na Uvuvi, Dk.Jackson Nkuba(kulia), akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu mkutano unaoendelea wa kujadili changamoto zinazoikumba secta ya Tumbaku unaofanyika katika Hoteli ya Lamada jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Rais wa Chama cha Wakulima wa Tumbaku Duniani, Daniel Green na Mtendaji Mkuu wa Chama hicho(CEO), Antonio Abrunhosa.
Mtendaji Mkuu wa Chama cha Wakulima wa Tumbaku Tanzania (Flue & Dark Tobacco Unio), Miraji Mgalula (kulia), akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu mkutano unaoendelea wa kujadili changamoto zinazoikumba secta ya Tumbaku unaofanyika katika Hoteli ya Lamada jijini Dar es Salaam.Wapili kushoto ni Mkurugenzi msaidizi wa Wizara ya Kilimo,Ufugaji na Uvuvi, Dk.Jackson Nkuba na Rais wa Chama cha Wakulima wa Tumbaku Duniani, Daniel Green.


Wakulima wa Tumbaku kutoka nchi mbalimbali wameziomba serikali zao kuweka  utataribu maalumu wa kuendesha mijadala katika nchi husika na wadau wake kimataifa, juu ya changamoto zinazokabili sekta hiyo, hali inayopelekea kushuka kwa mahitaji ya zao hilo kwa kutokuwapo na mazao mbadala.

Kushuka kwa mahitaji ya tumbaku kutasababisha baadhi ya nchi za Afrika kukumbana na tatizo la ajira na kupungua kwa kipato katika baadhi ya familia. Kunahitajika jitihada za ziada kwa wakulima wa tumbaku kuwa na zao mbadala, ambapo hadi sasa hakuna hatua zinazochuliwa kuwapa mwongozo wakulima.

Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam leo, katika mkutano wa wadau wa zao la tumbaku kutoka nchi mbalimbali, ulioandaliwa na Chama cha Wakulima wa Tumbaku cha Kimataifa (ITGA) na kuwashirikisha viongozi wa kisiasa na wakulima wa tumbaku kutoka   Malawi, Afrika Kusini, Zambia na Zimbabwe.

Akizungumza wakati wa mkutano huo, Rais wa ITGA Daniel Green, anasema, “Ninayo furaha kubwa kuwakaribisha wanachama wa ITGA hapa Tanzania katika mkutano huu muhimu wa vyama vya wakulima. Napenda kutambua mchango wa zao la tumbaku katika kukuza uchumi wan chi hizi, pamoja na kupita wakati mgumu. Kwa muda mrefu zao la tumbaku limechangia kwa kiasi kikubwa kutoa ajira katika nchi hizi na vile vile ni chanzo kikubwa cha kipato.

“Hatupingani na sharia zinazosimamia afya wa jamii. Jambo pekee ambalo tumekuwa tukilipigania ni kuwa sehemu ya mchakato ambao ungeweza kuwaongoza wakulima wa tumbaku kuwa na mkipango endelevu kwa usalama zaidi.

Kwa mujibu wa Green, nchini Tanzania, kilimo cha tumbaku kinatoa ajira 1.45 milioni na kuchangia kwa asilimia 5 ya mapato kwa kuuza bidhaa hiyo nje ya nchi.

“Kwa nchi ambazo zina huitaji mkubwa wa tumbaku, kama ilivyo kwa nchi za afrika, kunatakiwa kuwapo na mpango maalumu ambao unatakiwa kujadiliwa na wadau wote kwa pamoja. Bila kufanya hivyo, itakuwa vigumu kuendelea kuzalisha zao hili  kwa ujumla wake katika nchi husika,” alisema Green.

Katika hatua nyingine, wakulima wa zao hilo, walisisitiza suala zima la ushirikishwaji kupitia wawakilishi kwa kuzingatia ajenda ya Shirika la Afya Duniani (WHO) (Framework Convention on Tobacco Control ,FCTC). katika makubaliano yake juu ya matumizi ya tumbaku.

FCTC  inafanya mkutano jijini Dar es Salaam sambamba na ITGA kujadili hatua kadhaa kwa kuhusiana na vifungu vya 17 an 18 vya sharia, ambavyo moja kwa moja vinahusika na kilimo cha tumbaku na mchakato wake.

Mkutano huo unajadili mambo kadhaa ikiwamo njia mbadala za ukulima wa tumbaku na jamii kwa ujumla na yatokanayo na ukulima wa tumbaku ikihusishwa na mazingira.
 
Kwa mara nyingine tena, ITGA imetaka ushiriki wa chama chake hapa nchini (Flue and Dark Tobacco Unions,FDTU) katika mkutano huu, lakini kikikataa makubaliano yake kama iliyotajwa katika azimio katika mkutano wa mwisho wa vyama uliofanyika  (COP7) Delhi, ambapo Kiongozi wa kongamano  Vera Luiza Costa e Silva, alisema kuwa lengo lilikuwa ni kuwasaidia wakulima.

Ombi hilo lilikataliwa na wakulima pamoja na wawakilishi huku wakiendelea na mjadala juu wa mipango ya wakati ujao.

 António Abrunhosa, ITGA CEO alisema, “tumefikia wakati ambao tunaona kuwa sekretarieti ya FCTC , imekuwa na veto kwa wakulima wa tumbaku kwa kukataa maombi yao. Kama ilivyo kwa wakala wengine wa UN, ambao walihusika katika mijadala na wadau husika kujadili jinsi ya kufikia mafanikio.

FCTC imeshusha hadhi moja ya mdau wake muhimu katika mijadala yake, na mmoja wa waathirika wakubwa wa mijaqdala yake, ambaye ni jamii za wakulima wa tumbaku.”   

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad