HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 14, 2017

LIGI KUU MSIMU WA 2016/2017,MIZENGWE ILIZIDI.

Na Honorius Mpangala.

Wakati kipenga cha ufunguzi wa kigi kikipigwa agosti 20 mwaka 2016 kwa mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Azam na Yanga ilikua ni kitu kilichokua kikisubiliwa na wapenzi wengi kutokana na wadau kushuhudia usajili kabambe wa vilabu vyao.

Kuanza kwa ligi kuliweza kutoa harufu ya msisimko na ushindani katika msimu huo,mfano mechi ya kwanza kati ya Azam Fc dhidi ya African Lyon ilikua mechi ambayo iliwaduwaza sana mashabiki na benchi la ufundi la azam kutokana na shughuli waliyokutana nayo toka kwa vijana wa African lyon.

Azam katika mchezo huo ilisawazisha dakika za mwisho baada ya Lyon kutangulia kwa mpira wa kona ulioingia moja kwa moja na kumshinda kipa Aishi manula.

Kwa upande wa ratiba wadau wengi ambao wengi wao ni wanazi wa simba na yanga walilalamikia kwa kuona timu moja wapo ina pendelewa.

Changamoto ya ratiba imekua ni mfupa ulioshindikana kabisa kutokana ligi kusimama Mara kwa Mara au kutoa viporo kwa baadhi ya timu kutokana na kuwajibika kimataifa .

Mapendekezo yanayoweza kuwa bora ni uandaaji wa ratiba wa ligi kuu utazame kalenda ya FIFA  pamoja na ile ya CAF  ili wanapopanga wasiweze kuleta mkanganganyiko na kusababisha viporo.

Kwa upande wa usajili uliozua zengwe na kuleta mkanganyiko ni ule wa mchezaji Said mkopi aliyekuja kufungiwa baada ya Tanzania Prisons kupeleka pingamizi na kuonekana mkopi ana mkataba na klabu yake ya zamani huku akisajiliwa tena Mbeya City.

Maamuzi yalitotokea kwa Mkopi yalishindwa kutokea kwa mmoja wa Wachezaji wa African Lyon ambaye akikatiwa rufaa na klabu ya Yanga baada ya kuonekana alikua na pingamizi toka moja klabu ya ligi kuu nchini na mwisho wa siku TFF ilishindwa kufanya maamuzi hayo kwa wakati baada ya uchunguzi ilikuja kumfungia mchezaji huyo lakini pendekezo la klabu ya Yanga kupata point Tatu kutokana na mchezo huo haikufanyika.

Zengwe lingine ilikua ni usajili wa Hassan Ramadhan Kessy kutoka klabu ya Simba na kusaini klabu ya Yanga.

Picha la kessy lilianza kuwekwa wazi katika fainali ya FA msimu wa 2015/2016 iliyoikutanisha Azam fc na Yanga baada ya mchezo Kessy alijitokeza katika jezi ya yanga huku akilakiwa vyema na Mpinzani wake wa nafasi Juma Abdul Jaffary Mnyamani.

Mizengwe iliendelea kwani Tangu mwanzo wa msimu viongozi wa tff wakijikuta ktk wakati mgumu kwa kuwaondoa Geita Gold mine Fc na kuwapa nafasi Mbao Fc ambayo haikutarajia kucheza ligi kuu msimu uliomalizika.

Moja ya mambo ya kiufundi waliyokuwa wameiyafanya vilabu vya simba yanga na Azam yalikua na tija kwa vilabu hivyo kwani yalileta matokeo chanya mfano maamuzi ya azam kuachana na wahispania wale kulileta matokeo mazuri na kufanya klabu kufikia hatua ya NNE kwani kama wangeendelea kubaki na Wahispania wale kungeiangusha vibaya zaidi klabu ya Azam.

Kwa upande wa klabu ya simba maamuzi ya kumpa mkataba omog kulikua na faida kubwa kama ilivyokua kwa yanga kumbadilisha Mwalimu kulileta matokeo chanya pia.

Miongoni kwa kanuni zilizoshangaza wadau wengi ni lile sakata la kadi tatu za Novatus Lufunga na kadi tatu za Mohammed Fakhi zilizoleta mkanganyiko mkubwa na kukiuka taratibu za Mpira duniani.

Waweza kusema linaloshindikana Ulaya Tanzania linawezekana na watu wakalifungia Kazi na kuaminisha umma kuwa ni halali.

Kwa upande timua timua ya wachezaji hakuna mdau aliyetegemea golikipa wa Simba Vincent agban kama angekumbana na fagio la kuondoka klabuni au Jean Baptista Mugiraneza wa azam ambao walionekana kuwa ni wachezaji nguli kama ilivyokua kwa mbuyu twite wa yanga aliyempisha Justin Zulu.

Tabia ya mchezaji toka timu ndogo akiisumbua timu kubwa wakikutana ni kama anajipigia kampeni ya kusajiliwa imezidi kudhihirika kwani klabu ya yanga walifanya usajili wa Emmanuel Martin toka JKU ya Zanzibar kwa mtindo huo ,pia mchezaji Pastory Atanas mchezaji wa zamani wa stand utd alisajiliwa Simba baada ya kuifunga klabu ya yanga .

Uhamisho kwa upande wa Wachezaji wageni ilikua gumzo kwani ilikuja kuonekana kwamba klabu yeyote toka nje ya Tanzania iliyopata kuonyesha uwezo wake hapa nchini kulifanya vilabu kuwafuatilia na kuwasajili wachezaji hao. Hii ni moja ya Tabia za kitanzania ambapo viongozi wetu hawana muda wa kufuatilia wachezaji nje ila wanasubiri waje nchini ndipo wawaone hii inatoa maana kuwa hatuna uwezo mzuri wa kufuatilia wachezaji huko huko nje.

Azam na simba waligawana wachezaji wa Medeama ya Ghana Mara tu walipowaona wakikabiliana na Yanga hapa nchini.

Klabu ya mbao nikitegemea ingekuwa ndo klabu bora na hata kocha wao ingewezekana angekuwa kocha bora kutokana na mazingira waliyokua nayo mbao fc,moja ya sifa ambayo walikua nayo ni kutengeneza chemistry nzuri kuanzia eneo la mlinda mlango hadi ushambuliaji.

Ingeweza kusemwa kuondolewa kwa Kipa wa mbao Erick Ngwegwe kungeweza kuiathiri timu lakini mbadala wa ngwegwe ambaye ni Benedict Haule a.k.a Berko kuliwashangaza wengi na akamaliza msimu vyema.

Yako mambo ambayo vilabu vya majeshi vinaweza kujitathimini na kutazama ni mtindo upi wautumie katika kuwa na timu ligi kuu, wangeweza kuwa na klabu moja na kuitunza vyema na mishahara mizuri na kuweka falsafa ya kusajili hadi nje ya nchi katika kuimarisha vilabu vyao .

Simaanishi wachezaji wa ndani sio wazuri hapana ila najaribu kutazama namna watakavyo weza kubadili mifumo na kuwa vilabu vya kupambana kwaajili ya mataji na sio kufanya mchezo kwao ni kama ziada.

Nini kifanyike.

Pendekezo lililotolewa na uongozi yaani bodi ya ligi kwa kuhitaji maoni katika mapendekezo ya marekebisho ya kanuni ni moja ya kitu kizuri sana ambacho kitaweza kupunguza au kama sio kuondoa kabisa mikanganyiko inayojitokeza.

Kamati inayohusika na hadhi ya wachezaji wanatakiwa kufanya Kazi kwa weredi bila kusukumwa na upande wowote au mihemko ya watu Fulani.

Wachezaji ni bora wakajitambua na kuachana na uhuni wa kizamani ambao mwisho unakuja kukugharimu hili nalisema kutokana na lile lililomkuta Saidi Mkopi ambaye kajikuta anakaa nje kwa kutokucheza kabisa msimu mzima.

Klabu zijenge utamaduni wa kufanya mazungumzo na Klabu zingine pale inapofikia hatua kutaka kumchezaji toka klabu nyingine na kuachana na tabia ya kuzungumza na mchezaji ambaye mwisho wa siku klabu inaingia hasara ya kulipa faini kwa usajili wa kificho.

Yako mambo mengi ya kiswahili ambayo kamati ya ligi inapaswa kuyachunguza vyema hasa Yale ya klabu kutoingia katika vyumba vya kubadilishia nguo.

Ulinzi ulio bora kwa kutumia askari na sio mabaunsa katika vyumba ndio suluhisho la malalamiko ya vyumba kupuliziwa dawa kama madai yao yalivyo.

Kwa upande wa msisimko wa mashabiki uko juu sana na klabu vimekua vikitoa ushindani mkubwa,ni nadra kuona simba anashinda mchezo wa mbao kirahisi Kazi kubwa inafanyika mchezo wa yanga dhidi ya ndanda unakua na msisimko na usio kuwa na matokeo ya moja kwa moja hii inatufanya tuamini kuwa mpira wetu unapambana kutaka kuifanya ligi yetu na msisimko mkubwa.

Kila idara katika uongozi ikifanya vyema inatoa matokeo chanya vilevile hata vilabu vikiwa na viongozi wenye kusimamia kanuni toka shirikisho navyo vita kuwa na nidhamu na haitatokea mambo ya vilabu kuruka ukuta au kugomea zawadi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad