HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 19 June 2017

VIGOGO WA ESCROW NA IPTL WAPANDISHWA KIZIMBANI LEO


Taasisi ya kuzuia na kupambana Rushwa nchini (TAKUKURU),imewafikisha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu watu wawili James Rugemalira (Pichani kushoto) na Harbinder Seth Sigh (Pichani kulia) kwa tuhuma ya kesi ya Uhujumu Uchumi.

Akizungumza mapema leo mchana jijini Dar Es Salaam,Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini (TAKUKURU), Valentino Mlowola amesema kuwa Mmiliki wa VIP Engineering and Marketing, James Rugemalila na Mmiliki wa Kampuni ya IPTL, Harbinder Seth Sigh wamefikishwa mahakama ya Kisutu leo mchana kwa kosa la kuhujumu uchumi pamoja na makoasa mengine yanayofanana na hayo.

Mlowola amesema kuwa watuhumiwa hao wameshafikishwa mahakamani kwa kosa la kuhujumu uchumi pamoja na makosa yanayofanana na hayo,akaongeza kusema kuwa TAKUKURU wamechunguza shauri hilo kwa muda mrefu na sasa imefika wakati kuwapeleka mahakamani watuhumiwa hao kujibu mashtaka yao.

Mlowola ametoa Wito kwa wananchi kutambua kuwa serikali ina nia njema na dhati kabisa ya kuwapa Maisha bora Watanzania,hivyo hakuna budi wale wote wanaotuhumiwa kwa makosa mbali mbali watafikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Kabla ya vigogo hawa wawili kufikishwa mahakamani leo, baadhi ya watumishi wa TANESCO tayari walishtakiwa kufuatia tuhuma za kupokea fedha kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engeneering and Marketing ambaye pia alikuwa Mkurugenzi wa kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Ltd (IPTL), James Rugemalira.
Mmiliki wa VIP Engineering and Marketing, James Rugemalila na Mmiliki wa Kampuni ya IPTL, Harbinder Seth Sigh wakiwa wamechuchumaa kabla ya kupelekwa kwenye chumba cha mahakama kwa ajili ya kusomewa mashitaka yao,likiwemo la Uhujumu uchumi
Mmiliki wa VIP Engineering and Marketing, James Rugemalila na Mmiliki wa Kampuni ya IPTL, Harbinder Seth Sigh wakiwa ndani ya chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu tayari kwa kusomewa mashitaka yao,likiwemo la Uhujumu uchumi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad