HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 9, 2017

TAMISEMI : FFARS NI KIGINGI CHA WANASIASA KUZILALAMIKIA HALMASHAURI ZA WILAYA


Imeelezwa kuwa mfumo mpya wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma ‘Facility Financial Accounting and Reporting System – FFARS) utasaidia kuondoa malalamiko kwa wanasiasa kuzinyooshea halmashauri kuwa zinatumia vibaya mali za umma. 


Hayo yamesemwa leo Ijumaa June 9,2017 na Afisa Msimamizi wa Fedha Mwandamizi kutoka Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Elisa Rwamiago,wakati wa kufunga mafunzo ya siku mbili kuhusu mfumo wa FFARS kwa maafisa elimu kata na waganga wafawidhi katika vituo vya afya kutoka kata 18 za halmashauri ya Msalala wilaya ya Kahama mkoa wa Shinyanga,yaliyofanyika katika ukumbi wa Submarine Hotel mjini Kahama.
Rwamiago alisema wanasiasa wengi wamekuwa wakizitupia lawama halmashauri za wilaya kutumia vibaya pesa za serikali kutokana na kukosekana kwa uwazi na mfumo mzuri wa ukusanyasaji na utunzaji wa taarifa za fedha.
Alisema FFARS itasaidia katika kufuatilia matumizi ya fedha zinazotolewa na serikali katika kufikia malengo ya utoaji huduma na kuhakisha yanaendana na sheria ya manunuzi na utoaji taarifa, ili kuisaidia serikali kuimarisha mfumo wa usimamizi wa fedha za umma katika vituo vya kutolea huduma ikiwemo shule,vituo vya afya na hospitali za wilaya.
“FFARS ina faida kubwa kwetu kwani kukosekana kwa uwazi ilikuwa ni chanzo cha wanasiasa kusema katika halmashauri kuna mchwa hivyo mfumo huu utatutoa katika matumizi bubu ya fedha na kuwa ya wazi zaidi na tunategemea matokeo mazuri”,aliongeza Ramiago.
Naye Mhasibu wa Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo- Dodoma Bwanakheri Abdi Muhoma anayefanya kazi na mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma ‘ Public Sector Systems Strengthening – PS3’,alisema pesa za serikali zilikuwa zinatumika vibaya kutokana na kukosekana kwa mfumo unaofanana katika kukusanya na kuandaa taarifa za kifedha.
“Huu mfumo utasaidia sana kuongeza uwazi katika masuala ya fedha kwani pesa za serikali zilikuwa zinatumika kwenye matumizi yasiyo sahihi hivyo uwajibikaji utakuwepo kwa watendaji wa serikali”,alieleza Muhoma.
Kwa upande wake Mshauri wa Kifedha kutoka PS3,Osoro Otieno aliwataka maafisa elimu kata na waganga wafawidhi katika vituo vya afya walioshiriki mafunzo hayo kutoa elimu kwa watoa huduma wengine katika shule na vituo vya afya kwani FFARS inaanza kutumika kuanzia Julai 1,2017.
Nao washiriki wa mafunzo hayo waliipongeza serikali kuruhusu mfumo huo utumike ili kuongeza uwajibikaji na uwazi katika matumizi ya pesa za serikali.
FFARS inatekelezwa na mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma ‘ Public Sector Systems Strengthening – PS3’,Mradi wa Tuimarishe Afya ‘ Health Promotion and System Strengthening – (HPSS) unaofadhiliwa na watu wa Uswizi (Swiss Tropical and Public Health Institute) na TAMISEMI kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID). 
Afisa Msimamizi wa Fedha Mwandamizi kutoka Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Elisa Rwamiago akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya siku mbili kuhusu mfumo wa FFARS kwa maafisa elimu kata na waganga wafawidhi katika vituo vya afya kutoka kata 18 za halmashauri ya Msalala wilaya ya Kahama
Afisa Msimamizi wa Fedha Mwandamizi kutoka Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Elisa Rwamiago,akizungumza ukumbini
Mshauri wa Kifedha kutoka PS3,Osoro Otieno akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo
Mshauri wa Mifumo ya Kifedha kutoka PS3,Martin Lawi akisisitiza jambo wakati wa mafunzo hayo
Afisa Elimu Kata ya Chela,Matunda Hamza akichagia hoja wakati wa mafunzo kuhusu FFARS
Mshauri wa Mifumo ya Utawala Bora ma Ushirikishwaji wa Wananchi kutoka PS3,Dk. Chinuno Charles Magoti akiandika dondoo muhimu za mafunzo kuhusu FFARS kwa kutumia kompyuta
Wakufunzi wa mafunzo kuhusu FFARS wakiwa ukumbini
Mshauri wa Mifumo ya Kifedha kutoka PS3,Martin Lawi akitoa mwongozo kwa mshiriki wa mafunzo hayo kuhusu namna ya kujaza taarifa za masuala ya fedha
Washiriki wa mafunzo hayo wakichukua vitendea kazi kwa ajili ya kufundishia kwenye vituo vya kutolea huduma ikiwemo shule na vituo vya afya katika kata zao
Kulia ni Afisa Elimu kata ya Kashishi Ally Shaban Misana akipokea fomu kwa ajili kutolea mafunzo katika vituo vya kutolea huduma kwenye kata yake kutoka kwa Mhasibu wa Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo- Dodoma Bwanakheri Abdi Muhoma anayefanya kazi na PS3’.
Zoezi la kugawa vitendea kazi likiendelea
Mratibu wa HPSS halmashauri ya Msalala,Happiness Josephat akijiandaa kugawa vifaa vya kufundishia kwa washiriki wa mafunzo hayo
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa na vifaa vya kufundishia kuhusu FFARS kwenye vituo vya kutolea huduma katika kata zao.


Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad