HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 9 June 2017

TAIFA STARS KIBARUANI KESHO DHIDI YA LESOTHO.

Kocha Mkuu wa Stars, Salum Mayanga akiwa na Nahodha wa timu Mbwana Samatta wakati wa mahojiano na waandishi wa habari.


Taifa Stars watawakaribisha Mamba kesho kuanzia Saa 2:00 usiku Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza wa Kundi L kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2019.Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), limetangaza wamuzi wa mchezo kati ya Tanzania na Lesotho na kwa mujibu wa CAF, waamuzi hao ni Abdillah Mahamoud - atakayekuwa mwamuzi wa kati wakati wasaidizi wake ni Gamaladen Abdi na Farhan Bogoreth wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Twagirumukiza Abdoulkarim kutoka Rwanda huku Kamishna akiwa ni Amir Hassan wa Somalia

Kocha Mkuu wa Stars, Salum Mayanga amesema kuwa  timu imemaliza salama mazoezi na wana imani kesho watafanya vizuri.


“Timu imemaliza salama mazoezi leo asubuhi, hali za vijana ni nzuri na nina imani tutafanya vizuri na tutapata ushindi na tunaiheshimu Lesotho, kwa sababu ukiangalia mechi za nyuma zote wamefanya vizuri hivyo tutajitahidi kufanya vizuri kwenye mchezo wa kesho,”amesema Mayanga.


Taifa Stars itaingia kwenye mchezo wa kesho ikitoka kwenye kambi ya wiki moja nchini Misri na kwa ujumla huio utakuwa mchezo wa tatu kwa Mayanga tangu arithi mikoba ya Charles Boniface Mkwasa baada ya Machi mwaka huu kushinda 2-0 dhidi ya Botswana na 2-1 dhidi ya Burundi.

Nahodha  wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amesema kwamba kwa vyovyote vile kesho lazima washinde dhidi ya Lesotho.  Samatta anayechezea KRC Genk ya Ubelgiji amesema; “Afe kipa, afe beki lazima tuifunge Lesotho kesho,”


Jeuri ya Samatta kuwatangazia ubabe mapema Lesotho inatokana na maandalizi ya timu kwa ajili ya mchezo huo na zaidi anashukuru yeye kama Nahodha wa timu yuko vizuri kuelekea mchezo huo.

“Nimejiandaa vizuri kwa mechi ya kesho dhidi ya Lesotho na wachezaji wenzangu wote wapo vizuri na nina uhakika kambi walioiweka nchini Misri wamefanya mazoezi ya kutosha na tutafanya vizuri japo mechezo huu hautakuwa mwepesi,”amesema.

Hivyo sasa Viingilio katika mchezo huo vitakuwa ni Sh 10,000 kwa Jukwaa Kuu wakati mzunguko itakuwa ni Sh 5,000.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad