HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 15 June 2017

SPRITE BBALL KINGS KUENDELEA TENA WIKIENDI HII

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

MASHINDANO ya Sprite Bball Kings 2017 yanaendelea tena wikiendi hii kwa michezo mitano kupigwa katika Viwanja vya Bandari, Mivinjeni huku washindi wa jumla wa mechi hizo wataungana na wa wiki iliyopita.

Hii ni wiki ya tatu toka kuanza kwa mashindano hayo ikizikutanisha timu 52 kutoka sehemu mbaalimbali za Mkoa wa Dar es Salaam.Katika michezo ya wiki hii.

Katika wiki hii, kutakuwa na michezo mitano itakayowakutanisha Ukonga Warrior dhidi ya Mchenga Team, Heroes B dhidi ya Ardhi University na mechi ya tatu ni kati ya Flying Dribblers na UDSM.

Mechi ya nne ni kati ya Kigamboni Heroes na St Lous Montfort huku DMI wakivaana na nOsterbay michezo itakayoanza mida ya saa 2 asubuhi mpaka sa 12 jioni.


Mratibu wa mashindano hayo ya Sprite Bball Kings 2017 Basilisa Basike amesema hii ni muendelezo wa hatua ya pili baada ya wiki iliyopita kuchezwa kwa mechi nne na zingine tano zinamalizika wikiendi hii.


"Baada ya michezo hiyo, washindi wa jumla wataungana na wale wa wiki iliyopita na tutachezesha droo ya timu zitakazokutana ili kuingia hatua ya tatu ya Sprite Bball Kings 2017," amesema Basilisa.

Michuano hiyo inayodhaminiwa na Sprite kwa kushirikiana na East Africa Tv na Redio inaendelea tena wikiendi hii katika viwanja vya Bandari, Mivinjeni  na mshindi kamili ataondoka na kitita cha shiling milion 15.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad