HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 29 June 2017

WAZIRI MKUU, MAJALIWA KASSIM MAJALIWA :MAPAMBANO YA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA NI ENDELEVU

Na Chalila Kibuda, Dodoma
SERIKALI  imesema kuwa mapambano ya dhidi ya dawa za kulevya ni endelevu na wanaojihusisha kwa kusambaza hatua za kisheria zitachukuliwa.
Hayo ameyasema leo Waziri Mkuu ,  Majaliwa Kassim Majaliwa wakati wa kufunga maadhimisho ya siku kupiga vita dhidi ya dawa za kulevya Duniani iliyofanyika Mjini Dodoma, amesema kuwa vijana ndio nguvu kazi ya taifa kwa viwanda vinavyojengwa ikiteketea hakuna watu kutumikia viwanda hivyo.
Amesema kuwa Mamlaka ya Kidhibiti Dawa za Kulevya nchini ina mbinu za kisasa za kuwabaini watu wote wanaofanya biashara hizo.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa katika kipindi kifupi matokeo yameonekana kwa kuteketeza zaidi ya  ekari 565 za mashamba ya dawa za kulevya aina ya bangi.
Amesema Wakuu wa Mikoa bado wanaendelea kufichua na watu wanaojihusisha dawa za kulevya ikiwa ni nia ya serikali kumaliza kabisa tatizo hilo.
Amesema katika mwezi uliopita zaidi ya watanzania 1009 wako katika magereza nje nchi ambao wangetumika kuzalisha nchini lakini wanatmikia vifungo na wengine watanyongw.
‘’Yeyote anayetaka kudhohofisha nguvu kazi ya taifa letu ,anahujumu jitihada za ujenzi wa uchumi viwanda na anastahiki kushughulikiwa  bila huruma’’amesema Waziri Mkuu.
Nae Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera ,Bunge  Kazi, ajira na walemavu, Jenister Mhagama amesema kuwa asilimia 56 ya nguvu kazi ni vijana hivyo serikali iko imara katika kuhakikisha nguvu kazi hiyo inatumika.
Amesema kupitia ofisi yake kuna mipango mbalimbali ya kuwawezesha vijana ili waweze kutumika.
Waziri  Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza katika ufungaji wa maadhimisho ya siku ya dawa za kulevya iliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Sequare mjini Dodoma leo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera ,Bunge  Kazi, ajira na walemavu, Jenister Mhagama katika maadhimisho ya siku ya dawa za kulevya iliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Sequare mjini Dodoma leo.

Waziri  Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Life and Hope wa Sober House Bagamoyo , Al-Karim Bhanji wakati alipotembelea banda life and Hope katika kilele cha maadhimisho ya siku ya dawa za kulevya yalifanyika mjini Dodoma leo.
 .Waziri  Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Mawasiliano  na Uhusiano kwa Umma wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Gaudensia Simwanza wa  wakati waziri Mkuu alipotembelea Banda la TFDA katika maadhimisho ya siku dawa za kulevya yalifanyika Mjini Dodoma leo.
.Waziri  Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Naibu kamishina wa Idara ya Uhamiaji, Afisa Uhamiaji Mkoa wa Dodoma, Peter Kundy  wakati waziri Mkuu alipotembelea Banda la Uhamiaji katika maadhimisho ya siku dawa za kulevya yalifanyika Mjini Dodoma leo.
 ..Umoja wa waendeshaji wa vituo vya kuhudumia walioadhirika dawa za kulevya (VOS)wakiwa katika picha pamoja katika maadhimisho ya siku dawa za kulevya yalifanyika Mjini Dodoma leo.

 Sehemu ya wananchi wakiwa katika maadhimisho ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad