HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 29 June 2017

Kampuni ya Agricom Afrika na World Group Machine ya China zaingia makubaliano katika sekta ya kilimo

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Agricom Afrika, Angelina Ngalula (kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya World Group Machine ya nchini China, Buxin Wang wakati wakitambulisha mashine za kisasa za kuvunia mpunga, baada ya kuingia makubaliano ya kuwa wauzaji wa mashine hizo hapa nchini. Kampuni ya Agricom ni Kampuni ya kizalendo inayojihusisha na uagizani na uuzaji wa pembejeo za kilimo ikiwa ni zile za kulimia, kuvunia. Makubaliano hayo yamefikiwa leo Juni 29, 2017 katika ofisi zao zilizopo Mivinjeni, Kilwa Road jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Agricom Afrika, Angelina Ngalula (katikati) na ujumbe wake wakiwa katika mazungumzo na ujumbe wa  Kampuni ya World Group Machine ya nchini China ulioongozwa na Mkurugenzi wake, Buxin Wang, uliofanyika leo Juni 29, 2017 katika ofisi zao zilizopo Mivinjeni, Kilwa Road jijini Dar es salaam.
Picha ya pamoja baada ya mkutano wao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Agricom Afrika, Angelina Ngalula (wa tatu kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya World Group Machine ya nchini China, Buxin Wang wakati wakitambulisha mashine za kisasa za kuvunia mpunga, baada ya kuingia makubaliano ya kuwa wauzaji wa mashine hizo hapa nchini. Kampuni ya Agricom ni Kampuni ya kizalendo inayojihusisha na uagizani na uuzaji wa pembejeo za kilimo ikiwa ni zile za kulimia, kuvunia. Makubaliano hayo yamefikiwa leo Juni 29, 2017 katika ofisi zao zilizopo Mivinjeni, Kilwa Road jijini Dar es salaam. Wengine pichani toka kushoto ni Meneja Mipango wa Kampuni ya Agricom Afrika, Eric Mwidunda, Mkuu wa Kitengo cha Mauzo wa Kampuni ya World Group Machine ya nchini China, Jiayin Xu, Mtaalam wa Mashine hizo kutoka Kampuni ya World Group Machine ya nchini China, Yonghong Yu pamona na Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Agricom Afrika, Bernadetha Mariki.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad