Mtaa Kwa Mtaa Blog

WANAHABARI MBEYA WAJITOSA KUJILIPIA BIMA YA AFYA YA TAIFA (NHIF), RC MAKALLA AKABIDHI KADI ZA BIMA.

 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh, Amos Gabriel Makalla, amewapongeza waandishi wa habari mkoa wa Mbeya kwa uamuzi wao wa kuhamasishana kuchangia na kupatiwa kadi za bima ya Afya ya Taifa (NHIF).
Pongezi hizo zimetolewa katika ukumbi wa Coffee Garden mjini Mbeya alipokuwa akikabidhi kadi za bima ya Afya kwa baadhi ya waandishi wa habari Jijini Mbeya.
Makalla amesema waandishi wa habari wanafanya kazi kubwa katika Taifa na waandishi wa mkoa wa Mbeya wameamua kujitambua zaidi na kutambua kuwa matatizo hayaji kwa kupenda ikiwemo Kifo, Kuugua na uzee.
“Niwakumbushe wamiliki wa vyombo vya habari kuwawekea mazingira mazuri waandishi wao na kwamba kuna msemo unaosema kuwa ukondefu wa mbwa ni aibu kwa mwenye mbwa hivyo kutapatapa kwa waandishi wa habari ni aibu kwa wamiliki” alisema Makalla.
Aliomba waandishi kuendeleza uzalendo wao ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wananchi kujiunga na bima za afya ikiwemo mfuko wa bima ya afya ya jamii (CHF).
Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Mbeya Hoseah Cheyo alimwambia Mkuu wa mkoa kuwa pamoja na mambo mengine, waandishi wa habari wanampongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa kazi kubwa anazoendelea kuzifanya kwa ajili ya Taifa.
Katibu Mkuu wa chama hicho alisema kuwa waandishi wa habari wamehamasishana wenyewe katika kupata michango na kulipia kadi hizo.
Mwakilishi wa Mganga mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dr. Agness Buchwa, 
alisema kwa sasa Hospitali za mkoa wa Mbeya hususani Hospitali ya Mkoa na Rufaa, wametenga maeneo maalum kwa ajili ya watu wanaotibiwa kwa njia za kadi za bima ya Afya.
Mwakilishi wa Meneja wa mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa, Haji Mpeta alisema kuwa matibabu ni ghali hivyo waandishi waliolipia kadi za bima ya Afya wataweza kupata matibabu katika vituo 6500 kote nchini kwa gharama ya Tsh. 76,800 kwa mwaka.
 makamu Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Mbeya Hoseah Cheyo, akizungumza kwa niaba ya waandishi wa habari wa mkoa huo.
 Mwakilishi wa Mganga mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dr. Agness Buchwa, akizungumza na waandishi wa habari katika hafla fupi ya kuwakabidhi kadi za bima ya afya ya Taifa baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa Mbeya hawapo pichani..
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akimkabidhi kadi ya bima ya Afya  mwandishi wa habari Aines Thobias katika ukumbi wa Coffee Garden  uliopo Jijini Mbeya.
 Baadhi ya waandishi wa habari mkoa wa mbeya wakiendelea kudodosa matukio katika hafra fupi ya kupokea kadi za uwanachama wabima ya Afya 
PICHA ZOTE NA MR.PENGO MICHUZI MEDIA MBEYA.
MAELEZO NA GORDON KALULUNGA WA KALULUNGA BLOG
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.
  Post a Comment

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget