HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 8 June 2017

MSUVA AAHIDI USHINDI DHIDI YA LESOTHO JUMAMOSI

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Winga wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Simon Msuva amesema kuwa wanaamini watapata ushindi katika mchezo wao wa kufuzu kombe la Mataifa Afrika mwaka 2019 yatakayofanyika nchini Cameroon.

Taifa Stars inamenyana na timu ya taifa ya Lesotho mechi itakayopigwa siku ya Jumamosi majira ya saa 2 usiku kwenye Uwanja wa Chamazi.

Timu hiyo iliyoweka kambi ya wiki moja nchini Misri imerejea jana majira ya saa 6 mchana kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo.

Akizungumza na globu hii, Msuva amesema kuwa wao kama wachezaji wamefanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya mchezo huo siku ya Jumamosi na cha zaidi nawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi.

Msuva amesema kuwa, mechi hiyi ni muhimu sana ili kuweza kuweka matumaini ya kuingia fainali za Mataifa Afrika na watakachokifanya ni kuhakikisha wanapata ushindi.

"Tumejipanga kuhakikisha tunashinda katika mchezo wetu dhidi ya Lesotho ili malengo yetu yaweze kutimia na kuingia fainali za mataifa Afrika," amesema Msuva.

Winga huyo amesema kambi ya nchini Misri imeweza kuwajenga kiushindani na hata ukiangalia mazingira ya kule na hali ya hewa hakuna tofauti.

Stars inakabiliwa na mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi dhidi ya Lesotho utakaofanyika siku ya Jumamosi katika dimba la Uwanja wa Chamazi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad