HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 8 June 2017

AZAM TV WAINGIA MKATABA WA KUONYESHA MSIMU MPYA WA NDONDO CUP

 Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media Tido Mhando akikabidhiana mkataba wa makubaliano ya urushwaji wa matangazo wa michuano ya Ndondo Cup na Mratibu Shafii Dauda ukishuhudiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es salaam Almas Kisongo.                        

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

ILE michuano ya Ndondo Cup inatarajiwa kuanza kwa hatua ya makundi huku kituo cha kurushia matangazo ya Luninga ya Azam Tv wakidhamini kwa mara nyingine tena.

Utiaji wa saini wa mkataba wa kuonyesha michuano hiyo umetiwa leo baina ya Mratibu na Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media wakishuhudiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es salaam Almas Kasongo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media Tido Mhando amesema kuwa wanaipongeza Clouds Media kama w
aandaaji na waratibu wa michuano hiyo ya Ndondo Cup kwani imeweza kuwa na hamasa kubwa kwa vijana ambao wanapenda mpira na pia wanatumia kama fursa ya ajira.

Mhando amesema, wanaonyesha michuano hiyo kwa mara ya nne ikiwa mara ya kwanza walianza kwa kuonyesha hatua ya nusu fainali ila kuanzia msimu wa 2016 wameanzia hatua ya makundi.

Akizungumza kabla ya uwekaji wa saini wa mkataba huo, Mratibu wa michuano ya Ndondo Cup Shafii Dauda amesema kuwa huu ni mwaka wa nne toka kuanza kwa michuano hiyo na kampuni ya Azam Media wameweza kuionyesha na mwaka huu wameingia tena mkataba.

Dauda amesema, anawashukuru sana Azam Media kwa hatua hii kubwa ya kuonyesha tena michuano hiyo na wanaamini kuwa itazidi kuhamasisha kujiajiri kwa kucheza mpira wa miguu kwani kwa sasa inaonekana Afrika Mashariki na Kati.

Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguh Mkos wa Dar es salaam, Almas Kasongo amewapongeza Clouds Media na Azam media kwa hatu kubwa wanayoifanya ya kuhakikisha wadau na wapenzi wa Mpira wanaendelea kupata burudani.

Droo ya hatua ya Makundi itafanyika kesho katika fukwe za Escape One majira ya saa 8 mchana na kuweza kuzifahamu timu 32 zitakazoumana kumpata bingwa mpya wa michuano ya Ndondo Cup.
Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media Tido Mhando wakiweka saini mkataba wa makubaliano ya urushwaji wa matangazo wa michuano ya Ndondo Cup na Mratibu Shafii Dauda ukishuhudiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es salaam Almas Kisongo.                        

Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media Tido Mhando akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mkataba wa makubaliano ya urushwaji wa matangazo wa michuano ya Ndondo Cup kushoto ni  Mratibu Shafii Dauda na kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es salaam Almas KisongoNo comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad