HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 6 June 2017

HAKUNA WA KUTUZUIA KUPATA USHINDI MBELE YA SIMBA - NAKURU STARS

Mshambulaji wa kitanzania Jerome Nturukundo (kushoto) anayekipiga katika timu ya Nakuru Stars ya nchini Kenya.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Mshambulaji wa timu ya Nakuru All Stars Mtanzania Jerome Nturukundo amesema kuwa mechi yao dhidi ya Simba itakuwa ni ngumu sana ila watahakikisha wanafanya vizuri ili kuingia hatua ya nusu fainali.

Nakuru wanatakutana na mabingwa wa kombe la FA Simba katika mchezo wa mtoano utkaoafanyika leo saa 10:15 alasiri kwenye dimba la uwanja wa Uhuru.

Nturukundo amesema kuwa wanajua Simba ni timu nzuri sana lakinina wao wamekuja kupambana na kuhakikisha wanapata ushindi na kuingia hatua inayofuata.

"Tutajua simba ni team nzuri lakini na sisi  pia tunekuja kiushindani na wafahamu timu yetu imekamilika na leo wapo katika wakati mgumu kwa sababu  sisi pia tumekuja kushinda,"amsema Jerome

Kwa upande wa beki wa kati  James sadicky mukhwana yeye amesema kuwa ujio wao Tanzania ni kwa ajili ya kuhakikisha wanapat ushindi katika michezo yao na malengo yao ni kuona kombe la Sportpesa Super Cup likienda nchini Kenya.

"Simba wasifikiri itakua rahisi kuweza kuoata ushindi katika mchezo wetu wa leo kwani tunataka kombe liiende nyumbani Nchini Kenya na mimi kama mlinzi nitahakikisha hakuna makosa yatakayofanyika katika eneo langui,"amesema  mukhwana.  

Timu ya Nakuru inanolewa na kocha mzawa George Maina imekuja nchini katika michuano ya Sportpesa Super Cup iliyoandaliwa na kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Sportpesa.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad