HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 10 June 2017

DK. SHEIN ATOA MSAADA KWA WANANCHI WA PEMBA WANAOISHI KWENYE MAZINGIRA MAGUMU, WALIOATHIRIKA NA MAFURIKO

  MAGODORO 80 yaliotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Zanzibar, dk Ali Mohamed Shein, yakiwa kwenye uwanja wa jengo la Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba, kabla ya kugawiwa kwa waathirika wa mvua wa mkoa huo, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdalla, akiwakabidhi wakuu wa wilaya za Mkoani Hemed Suleiman Abdalla na Mkuu wa wilaya ya Chakechake Salama Mbarouk Khatib, kila wilaya magodoro 40, yaliotolewa msaada na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, dk Ali Mohamed Shein, kwa ajili ya aathirika wa mvua wa wilaya zao, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdalla, akiwakabidhi wakuu wa wilaya za Mkoani Hemed Suleiman Abdalla na Mkuu wa wilaya ya Chakechake Salama Mbarouk Khatib, kila wilaya magodoro 40, yaliotolewa msaada na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, dk Ali Mohamed Shein, kwa ajili ya aathirika wa mvua wa wilaya zao, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
MKUU wa wilaya ya Mkoani Hemed Suleiman Abdalla, akitoa neno la shukuran, mara baada ya kukabidhiwa magodoro 40 na Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdalla, kutoka kwa rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar dk Ali Mohamed Shein kwa ajili ya waathirika wa mvua, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

UNGA wa ngano polo 112, uliotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, dk Ali Mohamed Shein pmoja na Mchele na Sukari idadi kama hiyo, kwa ajili ya wananchi wa Pemba, wanaoishi kwenye mazingira magumu, ambapo chakula hicho ni sadaka, inayotolewa kila mwezi wa ramadhan na rais wa Zanzibar kwa ajili ya futari, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 MJUMBE wa kamati ya zaka na sadaka ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ndgu Haji Nassib Nyanya, akimkabidhi kwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdalla, mchele, sukari na unga wa ngano, chakuka chenye thamani ya shilingi milioni 40, ikiwa ni sadaka iliotolewa na Rais Zanzibar, kwa ajili ya futari ya wnananchi wanaoishi kwenye mazingira magumu kisiwani Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
MKUU wa Mkoa wa kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdalla akizungumza kabla ya kuwakabidhi wakuu wa wilaya ya Mkoani na Chakechake, saruji paketi 150 kila wilaya, zilizotolewa na Rais wa Zanzibar, kwa ajili ya wananchi waliokumbwa na mafuriko ya mvua ilionyesha hivi karibuni, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Mwanajuma Majid Abdalla, akiwakabidhi wakuu wa wilaya za Mkoani Hemed Suleiman Abdalla, na Mkuu wa wilaya Chakechake, Salama Mbarouk Khatib, saruji paketi 150 kila wilaya, iliotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar dk Ali Mohamed Shein, kwa ajili ya waathirika wa mvua, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad