HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 6 June 2017

BlackFox Models yaendelea kunasa wanamitindo

KAMPUNI ya Mitindo ya BlackFox Models inazidi kujitanua huku ikiwatengenezea fursa vijana kukuza vipaji vyao mbalimbali.

Hivi karibuni Kampuni hiyo ilifanya usahili wa wanamitindo mkoani Mwanza ambapo mamia ya vijana walijitokeza na kunolewa huku wakijipatia mikataba ya kufanya kazi na kampuni hiyo.

Lakini pia imewachukua washiriki wa Miss Ardhi University ambao walishika nafasi tatu bora katika shindano hilo.

Washiriki hao ni Glady John, Stella Ernest na Evodia Patrick.
Akizungumzia maendeleo ya kampuni hiyo Mkurugenzi Mtendaji wake, Atu Mynah, Aj alisema kuwa lengo kubwa ni kuwajengea uwezo vijana wakitanzania.

Alisema, amehakikisha kuwa anawasaka vijana wenye nia ya kuwa wanamitindo na kuwaendeleza hadi kufikia malengo yao huku akisisitiza kuwa anawanoa katika misingi yote ya uanamitindo.
Alisema, anawaendeleza katika vipaji vyao ikiwa ni sambamba na kuwapatia elimu ya fani hiyo kuanzia kibiashara, kisheria na kila kinachotakiwa kwa mtu kuwa Mwanamitindo.

AJ, kushoto akipitia profile za baadhi ya wanamitindo walioomba kushiriki kwenye usahili huo.

Meza ya majaji ikiendelea na mchakato wa kuwapata wanamitindo.

Aj, akizungumza na wanamitindo kadhaa waliofanikiwa kuchaguliwa ambapo alisikika akisisitiza suala zima la nidhamu.

Mmoja kati ya wanamitindo waliojitokeza siku hiyo.

Washindi wa nafasi tatu za juu kwenye shindano la Miss Ardhi 2017, wakikaribishwa kwenye Ofisi za kampuni ya BlackFox Modeling , Felister Paul maarufu kama Fifi (kulia) ambapo walisaini mkataba wa mwaka mmoja. Kutokea kulia ni Glady John, Stella Ernest na Evodia Patrick.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad