HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 28 June 2017

BAHANUZI ATEMWA MTIBWA, WASAJILI WENGINE WAWILI


Said Bahanuzi akimtoka kwa kasi beki mwingine wa JKT

TIMU ya Mtibwa Sugar imewatema wachezaji saba wakikosi hicho waliomaliza mikataba yao na kufanikiwa kusajili chipukizi wawili wapya ambao ni beki wa kati, Hussein Iddi na mshambuliaji Salum Ramadhani kw ajili ya msimu mpya wa mwaka 2017/18.

Katika wachezaaji saba walioruhusiwa kuondoka katika timu hiyo ni pamoja na aliyewahi kuwa mshambuliaji wa Yanga Said Bahanuzi baada kumaliza mkataba wake

Mkurugenzi wa Mtibwa Sugar, Jamal Bayser amesema kuwa beki Hussein Idd ametokea katika timu ya JKT Oljoro ya Arusha na Salum Ramadhani ametokea Polisi Morogoro na kila mmoja amesaini mkataba wa miaka miwili kila mmoja na ni matumaini ya Mtibwa Sugar watang’ara Manungu.

Pamoja na hayo, Bayser amesema kwamba wanatarajia benchi la Ufundi chini ya Kocha Mkuu Zubeiry Katwila kupandisha baadhi ya wachezaji kutoka katika timu ya vijana ya Mtibwa Sugar.

“Uongozi wa Mtibwa Sugar unaendelea kufanyia kazi mapendekezo ya benchi la ufundi, hivyo basi usajili bado unaendelea na nyota wengine wanatarajiwa kuingia makubaliano na Mtibwa Sugar wakati wowote kuanzia sasa,”amesema.

Aidha, Bayser amesema kwamba Mtibwa Sugar imeachana na Jaffary Salum Kibaya, Said Mkopi, Maulid Gole ‘Adebayor’, Said Bahanuzi, Vincent Barnabas, Ally Lundenga na Ally Shomary ambao wamemaliza mikataba yao.

Mtibwa inasifika mno kwa kuibua wachezaji chipukizi kutoka timu mbalimbali ndogo na wengine kupandisha kutoka kikosi chake cha vijana ambao baadaye hugeuka lulu na kugombewa na timu kubwa, hususan Simba na Yanga.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad