HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 20 April 2017

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI YAJIDHATITI KUKARABATI MIUNDOMBINU YA OFISI ZA BALOZI

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Susan Kolimba akijibu swali la Mhe. Raisa Adallah Musa Bungeni katika kipindi cha maswali na majibu mapema leo asubuhi, amesema kuwa Wizara kwa kutumia bajeti ya maendeleo ya Serikali na vyanzo vingine vya mapato inaendelea kutekeleza mkakati wa kurekebisha na kuboresha miundombinu ya Ofisi za Balozi na makazi ya watumishi wa ubalozini katika maeneo mbalimbali yenye uwakilishi Duniani. 
Mkakati huu unahusisha ukarabati wa majengo yaliyopo, ujenzi wa majengo mapya, sambamba na ununuzi wa majengo mapya. Mkakati huu unaanza kutekelezwa katika mwaka wa fedha ujao 2017/2018. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Susan Kolimba akijibu maswali kutoka kwa Waheshimiwa Wabunge katika Kikao cha Bunge kwenye kipindi cha maswali na majibu 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad