HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 5 April 2017

Washindi kumi wajinyakulia kitita cha Milioni 62 kutoka M-Bet

Vijana kumi kutoka mikoa mbalimbali nchini wamejinyakulia kitita cha shilingi Milioni 62, kupitia matokeo ya kubashiri mechi yanayoendeshwa na Kampuni ya M-bet.

Mmoja wa washindi kati ya kumi(10)akiongea na mtandao huu jana kwa niaba ya wenzake wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa hundi yao iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Godson Nzinyangwa (28)Mkazi wa Mkoa wa Arusha amewashauri watanzania wote hususani vijana wenzake wenye umri unaoruhusiwa kisheria kujitokeza kubashiri matokeo ya mechi mbalimbali kupitia Kampuni ya M-Bet.

"Nashukuru sana M-Bet kwa kuniwezesha kujikwamua kimaisha,kwani mimi ndoto yangu ni kuwa msanii mkubwa hapa nchini nitatumia fedha hizi kutimiza ndoto zangu za kuwa msanii wakimataifa kwani mtaji nimeupata tayari ndoto hii imetimia sasa", alisema Nzinyangwa.

Kwa upande wake, Msemaji wa M bet,Godluck Wambura aliwapongeza washindi hao na kutoa wito kwa wakina dada kujitokeza kushiriki katika mchezo huo kwani mbali na kushinda mchezo huo unachangamsha na akili pia alisema Wambura.
Mmoja kati ya washindi 10, Bw.Godson Nzinyangwa (kushoto) akikabidhiwa mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 62/- na Msemaji wa M bet, Godluck Wambura (kulia) kwa niaba ya wenzake walizojishindia kupitia mchezo wa kubahatisha wa Supper 12 unaoendeshwa na kampuni hiyo wakati wa hafla fupi ya makabidhiano hayo leo jijini Dar es Salaam.
Msemaji wa M bet, Godluck Wambura akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam ya kuwakabidhi hundi washindi 10 waliojishindia kupitia mchezo wa kubahatisha Supper 12 unaoendeshwa na M-bet. wengine pichani ni washindi wa kiticha cha shilingi Milioni 62, Amon Felix (kushoto) na Mshindi mwenzake, Ruben Mazoya (kulia) wakimsikiliza kwa makini 
Godson Nzinyangwa (katikati) ambaye ni mmoja wa washindi wa kitita cha shilingi Milioni 62 kupitia mchezo wa kubahatisha Supper 12 unaoendeshwa na M-bet akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari kwa niaba ya wenzake 10, wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya hundi yao leo jijini Dar es Salaam,kushoto ni Msemaji wa M bet,Godluck Wambura na mshindi mwenzake Ruben Mazoya.
Washindi 10 wakiwa na nyuso za furaha wakishikilia hundi yao yenye thamani ya shilingi Milioni 62 walizojishindia kupitia mchezo wa kubahatisha Supper 12 unaoendeshwa na kampuni ya M-bet wakati wa hafla fupi ya makabidhiano hayo leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad