HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, April 26, 2017

Wanafunzi wapigwa msasa wa elimu ya Usalama barabarani

Wanafunzi wa shule ya Msingi Ushindi iliyopo mikocheni B jijini Dar es salaam, Wamepatiwa mafunzo maalum ya elimu ya Usalama barabarani na jeshi la polisi la Usalama barabarani kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania PLC.
Elimu hiyo imetolewa leo ikiwa ni mwendelezo wa jeshi hilo na Vodacom Tanzania kutoa elimu hiyo nchi nzima,Wanafunzi walipata fursa ya kujifunza alama muhimu za barabarani na matumizi ya barabara na mambo muhimu ya kuzingatia kuwaepushia ajali wanapokuwa wanatumia barabara wakati wa kwenda na kutoka shuleni na matembezi mengineyo.

Akiongea kuhusiana na mafunzo ya elimu hiyo ya Usalama barabarani Afisa mnadhimu kutoka makao makuu ya jeshi hilo SSP, Tabita Makaranga ameipongeza kampuni ya Vodacom kwa kuunga mkono jitihada  za serikali katika kutokomeza ajali  za barabarani “Kwa kutoa elimu hii kwa watoto wadogo  waliopo mashuleni kwa kiasi kikubwa tutaweza kupunguza tatizo hili kwa kuwa wataendelea kukua wakijua matumizi sahihi ya barabarani na kwa upande wao ni rahisi kuelewa kuliko watu wazima.

Siku hii imekuwa muhimu kwa wanafunzi hawa kwani maisha yao yapo mikononi mwetu kwani ajali za barabarani zimekuwa ni janga la kitaifa na duniani kote ambapo taasisi mbalimbali zinazohusika na kupambana na ajali zinaendelea kulipigia kelele kwa Nguvu zote“Ni wakati wa kukumbuka sasa –Sema  Hapana kufanya uhalifu wa barabarani”.Alisema Makaranga

Naye Mkuu wa Mkuu wa kitengo cha Usalama barabarani na mahala pakazi wa Vodacom Tanzania PLC,Karen Lwakatare amesema kuwa suala la kuelimisha jamii kuhusiana na usalama barabarani ni  jambo ambalo kampuni ya Vodacom itaendelea kulivalia njuga kwa nguvu zote kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi na wadau wengine.

“Tatizo la ajali nchini ni kubwa na kila mwaka wananchi wengi hupoteza maisha kutokana na ajali za barabarani ikiwemo idadi kubwa ya watu kubaki wakiwa na ulemavu wa aina mbalimbali pia ajali zinaathiri familia nyingi kutokana na wategemezi katika familia kupoteza maisha ama kupata ulemavu kutokana na ajali hususani za barabarani”.

Alisema tatizo hili ili kulitokomeza linahitaji ushirikiano wa watu wote “Vodacom tumekuja na mikakati mbalimbali ya kufanya kampeni hizi mojawapo ikiwa kupeleka elimu ya usalama barabarani kwa watoto wadogo waliopo mashuleni kama tulivyofanya leo na mkakati huu unaendelea kutekelezwa katika mikoa mbalimbali”.Alisema.

Lwakatare alisema mbali na elimu mashuleni Vodacom kwa kushirikiana na serikali kupitia Jeshi la Polisi na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani imekuwa ikiendesha kampeni ya “Wait to Send” ambayo inahamasisha  madereva wanaoendesha vyombo vya moto kutotumia simu za mkononi wanapokuwa barabarani na kutotumia vinywaji vyenye kilevi wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto kwa ajili ya kulinda usalama wao,abiria wanaowabeba na watumiaji wengine wa barabara.
Mwanafunzi wa shule ya msingi Ushindi Mikocheni B jijini Dar es Salaam, Issa Abdallah (kushoto) akiwasomea wanafunzi wenzake bango lenye ujumbe wa Usalama barabarani wakati wa mafunzo maalum ya elimu ya Usalama barabarani yaliyoendeshwa na Jeshi la polisi la Usalama barabarani kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania PLC.
Mwanafunzi wa shule ya msingi Ushindi Mikocheni B jijini Dar es Salaam,Emanuel Andrea (kulia) akiwasomea wanafunzi wenzake bango lenye ujumbe wa Usalama barabarani wakati wa elimu ya mafunzo maalum ya Usalama barabarani yaliyoendeshwa na Jeshi la polisi la Usalama barabarani kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania PLC.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Ushindi Mikocheni B jijini Dar es Salaam pamoja na Mkuu wa kitengo cha Usalama barabarani na mahala pakazi wa Vodacom Tanzania PLC,Karen Lwakatare(wakwanza katikati)wakimsikiliza Askari wa Jeshi la Usalama barabarani CPL,Faustina Ndunguru(kulia) akiwafundisha alama za barabarani wakati wa mafunzo maalum ya kuvuka barabara kwa wanafunzi hao yaliyoendejeshwa na jeshi hilo kwa kushirikiana Vodacom Tanzania leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad