HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 25, 2017

Simbu arejea nyumbani, aahidi kujipanga upya kwa mashindano ya Agosti!

Balozi maalum wa DStv na Mwanariadha pekee wa Tanzania liyeshiriki mashindano ya London Marathon Alphonce Simbu amerejea nyumbani na kutoa onyo kali kwa wale atakaokabiliana nao kwenye mashindano yajayo ya dunia  yatakayofanyika mwezi Agosti jijini London.

Simbu ambaye alishika nafasi ya tano katika mashindano hayo na kujishindia kitita cha dola za marekani 10,000 aliwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro na kulakiwa na maafisa mbalimbali akiwemo Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania Johnson Mshana, Meneja wa mwanariadha huyo Francis John.
 Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Arusha muda mfupi baada ya yeye kuwasili Simbu aliwashukuru sana watanzania wote kwa moyo wao na jinsi walivyomuunga mkono na kumtakia kila la heri katika mashindano hayo. Amesema alifarijika sana na pia kupata moyo zaidi alipokuwa akipokea salamu kutoka kwa watanzania kote ndani nan je ya nchi.

Akizungumzia mashindano hayo, Simbu amesema yalikuwa na changamoto kama yalivyo mashindano mengine makubwa ya kimataifa kwani yalishirikisha vigogo ambao wengi wao wana uzoefu mkubwa katika mashindano mbalimbali na wengine pia ni washindi wa mashindano ya hapo awali.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ambaye aliwakilishwa na mkuu wa Wilaya ya Monduli Idd Kimanta alisema mkoa mzima wa arusha umepokea kwa Furaha habari za mkazi wao kufanya vizuri katika mashindano makubwa kama hayo na kwamba wataendelea kushirikiana na Simbu na kumsaidia kwa kadiri itakavyowezekana ili kumuwezesha kuendelea kuuwakilisha vizuri mkoa na taifa kwa ujumla kwenye michuano ya kimataifa.

Amesema kuwa ushindi wa simbu uwe ni chachu kwa vijana wengine wa kitanzania wenye vipaji na wasibaki nyuma bali wajitokeze na watie nguvu katika kuonyesha vipaji vyao. “Tuna vipaji vingi sana tena siyo kwa riadha tu, bali vya kila aina, cha mshingi ni kushirikiana kwa karibu na wadau ili kuhakikisha vipaji hivyo vinaibuliwa na kuendelezwa kwa manufaa ya taifa kwa ujumla” alisema mkuu huyo wa mkoa.
Naye Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania Johnson Mshana amesema wao kama wadhamini wa Simbu wamepokea kwa Furaha kubwa matokeo hayo ambayo yanaonyesha kuimarika kwa kiwango cha Simbu. “Tuliamua kumdhamini Simbu tukiamini kabisa kuwa atakuwa nyota na atailetea Tanzania sifa. Tuna dhamira kubwa nay a dhati kabisa ya kuhakikisha kuwa siku moja wmbo wetu wa taifa unapigwa katika mashindano ya Olimpiki. Bila shaka hili lipo karibu kutokea”.alisema Mshana

Multichoice Tanzania inamdhamini Simbu kwa muda wa mwaka mzima kwa lengo la kufanikisha maandalizi yake ya kushiriki katika mashindano ya Dunia ya mwaka huu. Udhamini huu ulianza tangu mwaka 2016 ambapo Multichoice humpatia Alphonce posho ya kujikimu pamoja na kusaidia kambi yake ya mazoezi.
Alphonce, ambaye ni Mtanzania wa kwanza kushinda medali ya dhahabu katika mashindano maarufu ya Standard Chartered Mumbai Marathon, anatarajiwa kushiriki mashindano ya riadha ya dunia yatakayofanyika London mnamo mwezo Agosti mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad