HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 25, 2017

SIMBA YAIFUATA DAWA YA KUIA AZAM JUMAMOSI KOMBE LA FA

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

KIKOSI cha timu ya Simba kimeendelea kujifua kwa nguvu wakijiandaa na mchezo wa nusu fainali dhidi ya Azam utakaofanyika mwishioni mwa wiki hii.

Jumamosi ya April 29, ni nusu fainali ya kwanza ya kombe la Shirikisho la Azam HD baina ya Simba na Azam itakaopigwa katika dimba la Uwanja wa Taifa.

Kwa sasa Simba wapo Morogoro wakijiandaa na mchezo huo ambapo chini ya Kocha Joseph Omog na Jackson Mayanja kimeamua kujichimbia huko kwa ajili ya kuwapa muda wa kupumzika wachezaji wake na kuwapa mbinu mpya mbalimbali.

Hii inakuwa ni mechi ya ushindani mkubwa sana kwa timu hizi mbili zikikutana kwa mara ya tatu ndani ya msimu mmoja ambapo katika michezo miwili ya awali ila mmoja akishinda mchezo mmoja.

Kwa mujibu wa Kiongozi wa Simba, Abbas Ally amesema kuwa wachezaji wana ari kubwa sana na wako vizuri na wanaamini watapigana mpaka mwisho ili kupata ushindi kwenye mchezo huo.

"Huu ni mchezo muhimu sana kwetu, ni muhimu kupata ushindi  ili tuweze kuingia fainali ya kombe la Shirikisho na wachezaji wana ari kubwa sana ya ushindi na wameahidi kupambana mpaka mwisho,"amesema Ally.

Mpaka sasa Kikosi cha Simba kinakabiliwa na majeruhi wawili ambao wanatarajiwa kuukosa mcheoz huo ambao ni Hamad Juma na Jamal Mnyate.
Wachezaji wa Simba wakiwa katika mazoezi ya pamoja kulekekea mchezo wao wa nusu fainali ya kombe la Shirikisho la Azam HD siku ya Jumamosi dhidi ya Azam.



 Golikipa Peter Manyika akiwa katika mazoezi  kulekekea mchezo wao wa nusu fainali ya kombe la Shirikisho la Azam HD siku ya Jumamosi dhidi ya Azam.
 
 Wachezaji wa Simba wakimsikiliza Kocha Joseph Omog katika maandalizi ya mechi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam HD siku ya Jumamosi.
Wachezaji wa Simba wakiwa katika mazoezi ya pamoja kulekekea mchezo wao wa nusu fainali ya kombe la Shirikisho la Azam HD siku ya Jumamosi dhidi ya Azam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad