HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 25 April 2017

Serikali yamuondoa Mkurugenzi wa UNDP nchini

Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Programu ya Maendeleo (United Nations Development Programs – UNDP), Bi. Awa Dabo aliyeondolewa nchini.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeliagiza Shirika la Umoja wa Mataifa la Programu ya Maendeleo (United Nations Development Programs – UNDP) kwa upande wa Tanzania kumuondoa nchini Mkurugenzi wa Shirika hilo Bi. Awa Dabo.

Serikali ilifikia uamuzi huo kutokana na  Bi. Dabo kutokuwa na maelewano mazuri na baadhi ya Watumishi wenzake na Menejimenti ya Shirika hilo, hivyo kupelekea kuzoretesha utendaji wa shirika hilo nchini na kupunguza kasi ya kuleta maendeleo kwa Watanzania endapo hatua za haraka zisingechukuliwa.

Baada ya kuthibitishiwa kuondoka nchini, Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje imetoa rai kwa UNDP kuwakumbusha Watumishi wake kuwa kipaumbele chao ni kufanya kazi na Serikali ili kufikia malengo yaliyoainishwa kwenye Dira ya Maendeleo ya Mwaka 2025, Mpango wa Maendeleo wa Miaka mitano na Malengo ya Maendeleo Endelevu ambayo yamefafanuliwa katika Agenda ya Mwaka 2030.
  
Mwisho.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasilino ya Serikali kwa Umma,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma, 25 Aprili, 2017.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad