HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 18, 2017

PROFESA MKUMBO ATINGA DAWASCO AWAMWAGIA SIFA LAKINI AWATAKAKUONGEZA USAMBAZAJI WA MAJI,AZINYOSHEA VINDOLE TAASISI SISIZOLIPA ANKARA ZA MAJI.

 Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo akizungumza na waandishi wa habari na watendaji wa Dawasco baada ya kupokea taarifa ya huduma ya maji jijini Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco, Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza machache katika mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo (wa kwanza kulia) akiwa ameambatana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco, Mhandisi Cyprian Luhemeja (wa kwanza kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Mhandisi Archard Mutalemwa (katikati) kuelekea katika chumba cha mkutano baada ya kuwasili makao makuu ya Dawasco jana kupokea taarifa ya huduma ya maji jijini Dar es Salaam na Pwani.
waandishi wa habari na watendaji wa Dawasco wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo  leo jijini Dar es Salaam.Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.


KATIBU mkuu  wa Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo amesema  kuwa hakuna sababu ya  taasisi za Serikali kushindwa kulipa bili ya maji wakati taasisi hizo zinapewa fedha kutokana serikalini  na yeye kama katibu aliyepewa dhamana hiyo atahakikisha shirika  hilo linaongeza uwezo wa  kuhudumia wananchi.
Profesa Mkumbo amesema hayo leo katika ziara yake ya kwanza  ya kikazi katika shirika hilo, ambapo pamoja na mambo mengine aliipongeza Dawasco kwa kazi kubwa wanayoifanya  kwani  ukilinganisha na huko nyuma ambapo malalamiko ya maji  yamepungua kwa kiasi kikubwa.
Mkumbo amesema haiwezikani  mwananchi wa kawaida  anamudu kulipa  bili ya maji alafu taasisi za serikali ambazo zinapewa fedha zinashindwa kulipa hivyo lazima wahakikishe wanalipa na Dawasco wanatakiwa wafanye kazi hiyo ya kukusanya bili hizo za maji.
‘’ Nawapongeza  Dawasco  kwani mnafanya kazi kubwa  binafsi nimekuwa nikiwafuatilia hata kabla sijaingia wizaani kwakweli mnafanya kazi kubwa na mnastahli kupongezwa  lakini muendelee hivyo na kwakweli wananchi wanataka maji si vinginevyo.’’ Amesema   mkumbo
Pia alisema pamoja na kazi kubwa nakudai kuwa watoke kwenye lengo  badala yake  wahakikishe tatizo la maji linakwisha kabla ya kufika 2020  kwani kuna miradi mikubwa mno ya maji ambayo inatekelezwa na kwakweli kama ikikamilika basi shida ya maji itakuwa limepata suluhisho.
Mkumbo ameiongeza kuwa lazima shirika litoke kwenye mtazamo na kuingia kwenye uhalisia  n hiyo ndiyo kazi kubwa  iliyopo  na hapo nikuona watu wanapata maji  huku kibainisha maeneo kama Bonyokwa,Pugu,Chanyanyikeni Kinyerezi, maeneo hayo kwa kiasi kikubwa yanakabiliwa na Changamoto kubwa ya maji nay eye kama Katibu amepongeza Dawasco kwa kuliona hilo.
 Akiwasilisha  wake  kwa katibu huyo Ofisa Mtendaji mkuu wa Dawasco  Sypriani Luhemeja alisema kuwa shirika hilo limepiga hatua kubwa ukilinganishana na huko nyuma ambapo uzalishaji ulikuwa chini.
Amesema hivi sasa Dawasco wanazalisha lita milioni 480 kwa siku na hitaji ni milioni 512  na kudai kuwa kiwango hicho ni kikubwa ukilinganisha na huko nyuma na kwamba bado wamejipanga kikamilifu kuhakikisha kwamba wanamaliza tatizo la maji katika mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.
Aidha alifafanua kuwa uzalishaji wa maji  katika ruvu chini ni lita milioni 217, ruvu juu lita mil 196  na kutoka mtoni lita 9000 na vyazo vinginevyo vinachangia kwa asilimi ndogo  huku akibainisha kuwa jumla ya wateja  187,087  wamehudumiwa  na lengo nikuwafikia wateja 400000, ifikapo mwezi  juni 2017.
  Akizungumzia Changamoto Luhemeja alisema ni usambazaji wa maji pamoja na upotevu wa maji  ambapo katika kipindi cha mwaka 2015 maji yalipotea kwa asilimia 57 na kufikia mwezi machi mwaka huu maji yamepotea kwa asilimia 37.8.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad