HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 18 April 2017

MIAKA 20 IMEPITA, YANGA BADO ILE ILE

1998, Yanga ilifuzu kwa hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa. Walipangwa kundi B sambamba na Asec Mimosas ya Ivory Coast, Raja Casablanca ya Morocco na Manning Rangers ya Afrika Kusini.


Mchezo wao wa pili ulikuwa ugenini dhidi ya Asec, ulipigwa mpira mwingi mno japo Yanga walipoteza 2-1. Baada ya hapo walitakiwa waende Morocco kucheza na Raja Casablanca. Tiketi zao za ndege ziliandikwa ndege itaondoka Jumanne saa sita usiku. Basi wao wakaitafsiri kwamba walale Jumatatu halafu waamke Jumanne ndiyo usiku wake waondoke...kumbe Jumanne saa sita usiku ni baada ya saa tano usiku ya Jumatatu. Wao.walipoenda Jumanne usiku, wakaambiwa ndege imeondoka usiku uliopita, wakachelewa.

Ndege nyingine ya kwenda Morocco itakuja Jumanne ijayo saa sita usiku. Ikabidi wabaki Ivory Coast mpaka hiyo Jumanne. Ukikutana na mchezaji wa Yanga aliyekuwpo kwenye kikosi kile, akikuhadithia maisha waliyoishi kule tatamani kulia. Haikushangaza walipoenda Morocco wakafungwa 6-0 na Raja Casablanca.

Hatua ya makundi iliendelea na mechi ya mwisho Yanga waliwakaribisha Asec Mimosas uwanja wa Taifa(siku hizi Uhuru). Katika mchezo huo ulioisha kwa kipigo cha 3-0, Yanga walivaa jezi za Taifa Stars kwa sababu jezi zao zilifanan na zile za Asec. Makosa mengine(ila sijui ni ya nani). Pichani hapo, beki wa Yanga, John Mwansansu, akikabana na Abou Dominique wa Asec.

2017, Yanga wanafanya makosa yale yale ya 1998, wanachelewa ndege na kuwalazimu kubaki ugenini wasijue waanzie wapi. Wakitoka huko wana mchezo dhidi ya TZ Prisons robo fainali ya kombe la Shirikisho la Azam Sports. Endapo watapoteza mchezo huo kutokana na uchovu, viongozi hawawezi.kukwepa lawama.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad