HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 27 April 2017

MCHEZO HUU NI MGUMU SANA, HAUWEZI KUWA RAHISI KWETU - HIMID MAO


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

NAHODHA Msaidizi wa klabu ya  Azam Himid Mao ‘Ninja’, ameweka wazi kuwa wana morali kubwa ya kupata matokeo mazuri kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Sports) dhidi ya Simba utakaopigwa siku ya Jumamosi.

Mchezo huo wa nusu fainali ya kwanza kati ya Simba na Azam utapigwa katika dimba la UWanja wa Taifa ukichezeshwa na mwamuzi Mathew Akrama kutoka Jijini Mwanza na unatarajiw akuwa moja ya mechi ngumu sana kwa kila upande.

Kikosi cha Azam FC kipo kwenye maandalizi makali kuelekea mchezo huo, ambapo tayari kimeshaingia kambini mapema wiki hii  katika makao makuu ya klabu hiyo ndani ya viunga vya Azam Complex kujiandaa na mchezo.

Himid amesema  kikosi chote cha wachezaji wana ari kubwa na wapo vizuri  na watanufaika na urejeo wa wachezaji wao muhimu waliokuwa majeruhi.

“Morali iko juu, timu ipo vizuri bahati nzuri wachezaji wenzetu karibia asilimia 90 wapo vizuri na wapo fiti na wako tayari kwa mchezo na naamini kocha atakuwa na nafasi nzuri ya kuchagua timu yake ya kwenda kucheza mchezo huo,” alisema Mao.

Kiungo huyo wa timu ya Taifa alisema kuwa mchezo huo utakuwa mgumu licha ya kufanikiwa kuwafunga mara mbili katika mechi mbili zilizopita.

“Usidhani kama mchezo huu wa tatu utakuwa mrahisi kama mara mbili zilizopita tulizoshinda, kwani Simba nayo inajipanga, lakini naamini sisi tutajipanga vizuri zaidi ili kuweza kushinda mechi hiyo inayokuja,” alisema.

Himid ambaye amekulia kwenye timu hiyo kwa takribani miaka tisa sasa, alitoa wito kwa mashabiki wa Azam FC kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo huo ili kuwapa sapoti kwani wao ni sehemu muhimu sana katika timu na uwepo wao utawaongezea nguvu zaidi uwanjani ya kuibuka kidedea.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad