HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 27, 2017

UPENDO WOMEN’S GROUP WATOA MSAADA KATIKA WODI YA WAZAZI HOSPITALI YA MWANANYAMALA.

Umoja wa Wanawake Watanzania waishio nchini Ubeljiji, ‘Upendo Women’s Group’ leo wametoa msaada wa vifaa vya kwenye wodi ya wajawazito ya Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar.


Akizungumza na wanahabari leo wakati wanakabidhi vifaa hivyo, Mwenyekiti wa Upendo Women’s Group, Theresia Greca amesema kuwa changamoto wanazokutana nazo wanawake wa Kitanzania katika wodi mbalimbali wanazokwenda kujifungua ikiwemo uhaba wa vifaa na changamoto nyingine nyingi.

“Wajawazito wana changamoto nyingi sana wakati wa kujifungua, vifaa ni vichache, wahudumu wachache na changamoto nyingine nyingi, hivyo kama Upendo tumekuwa tukikusanya misaada kwetu na wadau mbalimba kwa ajili ya kusaidia wodi ya wajawazito ya Mwananyamala.

“Hii ni awamu ya tatu kwa Upendo kutoa vifaa kwenye wodi ya wazazi hapa Mwananyamala, leo tunatoa vifaa vifuatavyo: Fetal dopler 1, Speculum- SIMS 3, Speculum-cusco 3, Drum (medium)2, Mackintosh Troll 2, Penguin Sucker 2, Needle Holder 10, Sponge Forceps 10, Ambulance Stretcher 1, Ambubag Infant 2, Clinical Thermometer 30, NGT size 8, Drip Stand 3.

Vingine ni Vacuum Extractor 1, Bed Powder Coated 2, Double Step Powder Coated 6 Istrument Trolley 1, Ressuciatian Trolley 1 ambapo vifaa vyote vimegharimu T.Sh.s Mil. 10310000/= (Milioni kumi na laki tatu na elfu kumi).”

Umoja huo unaundwa na wanawake 14; akiwemo mwenyewe, Theresia Greca, Begum Razafinjatovo na Upendo Shoo ambao ni Waweka Hazina. Wengine Ni Fausta Mneney, Dora Maiga, Rosi Kadaga, Linda Shayo, Agnes Kayola, Sedda Maiga, Kimwisho Mndolwa, Hadija Juma, Imbori Na Editha.

Aidha Upendo imewataka Watanzania kujenga utaratibu wa kuwasaidia wodi za wazazi nchini na pia wamewashukuru sana wadau ambao wamekuwa wakishirikiana nao katika kufanikisha misaada hii akiwemo Rais wa Awamu ya Tatu, Mhe. Benjamin Mkapa, Begum Razafinjatovo, Rosi Kadaga, Chental Ramialimanana,”alisema Grace.

 Mweka Hazina wa Upendo Women’s Group ,Begum Chunny akizungumza wakati wanakabidhi vifaa mablimbaali katika Hospitali ya Mwananyamala leo jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Upendo Women’s Group, Theresia Greca na Mweka Hazina,Begum Chunny kwa pamoja wakikabidhi vifaa hivyo hivyo kwa Afisa Muuguzi wa Hospital ya Mwananyamala,Musa Wambura leo jijini Dar es Salaam.

Muonekano wa Vifaa hivyo vikiwa katika Hospitali ya Mwananyamala leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad